Monday, June 12, 2017

ARUMERU YANUFAIKA NA MITAMBO YA KISASA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA TAHADHARI


Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari (hawapo pichani) walipotembelea kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo Wilayani Arumeru Juni 09, 2017. 
Baadhi ya wakazi wa Vijiji vya Mbuguni Wilayani Arumeru wakimsikiliza Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei (hayupo pichani) wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu 09Juni, 2017. 
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha akizungumza na wakazi wa Mbuguni Arumeru wakati wa Tathimini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari iliyofanywa na ofisi yake June, 2017.
Mmoja wa wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bi. Mariam Daudi (Mkulima) kutoka Kijiji cha Makiba Wilaya ya Arumeru akionesha simu aliyopewa na mradi huo inayosaidia kupokea taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa wakati wa mkutano wa tathimini ya utekelezaji wa mradi eneo la Mbuguni Meru. 
Bi. Elizabeth Laiza kutoka Kijiji cha Shambarai Arumeru akieleza faida za mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa timu ya tathimini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (haipo pichani). 
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma vifaa vya kupima kina cha maji kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha 
Muonekano wa Vifaa vya kisasa vya kupima kina cha maji vilivyofungwa na mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika mto Kikuletwa Kijiji cha Kikwe Meru ambavyo husaidia katika taarifa za utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari ya mafuriko. 
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri akizungumza jambo wakati wa mkutano na Timu ya Ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 2017.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments: