Sunday, May 14, 2017

WAZAZI WATAKIWA KUWAEPUSHA WATOTO NA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.



Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule hiyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akioneshwa baadhi ya jumbe zilizopo katika mabango zilizoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongozwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Bi.Neema Daniel iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama kupanda mti wa kumbukumbu, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria kuanza kwa mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Deodatha Makani akiongea jambo na Mkurugenzi wa Ubora na Maendeleo wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo aliwataka wazazi kuwalinda watoto na ndoa za utotoni pamoja na kuwasisitiza kuendeleza vipaji vyao. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akitoa vyeti pamoja na zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita ya shule hiyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama pamoja na walimu wao. 
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia mahafali. 

…………………………………………………………………… 

Na Hassan Silayo-MAELEZO 

Wazazi nchini wametakiwa kutekeleza wajibu wao kwa watoto kwa kuhakikisha wanawaendeleza na kuwawezesha wafanikishe ndoto zao kwa kuwaepusha na ndoa pamoja na mimba za utotoni. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga katika Mahafali ya 5 ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama. 

Bi.Sihaba amesema kuwa wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawalea na kuwalinda kwani wazazi wanahaki ya kisheria ya kuwalinda watoto dhidi ya viashiria vyote vinavyoweza kuwaweka katika mazingira hatarishi. 

Bi.Sihaba aliongeza kuwa wazazi na walezi wana haja ya kushirkiana na serikali katika kuwalinda watoto wakike kwani watoto wa kike ni nyenzo muhimu hasa kwenye mpango wa serikali katika kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda. 

Aidha,Bi.Sihaba kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Elimu sura namba 33 inayotoa katazo kumpa ujauzito motto wa shule chini ya miaka 18 hivyo wazazi wahakikishe wanalisimamia kwa pamoja ili kuweza kufanikisha sheria. 

Naye Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake ili kuendana na mipango ya serikali ya awamu ya tano katika kuipa kipaumbele sekta ya elimu. 

Mkurugenzi wa Ubora na Maendeleo wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot amesema kuwa mahafali hayo ni ishara ya ushirikiano mzuri wa wazazi,walezi pamoja na uongozi wa shule utakaowezesha watoto hao kuvuna kile walichokipanda kwenye miaka 6 ya masomo yao. 

Mkuu wa shule hiyo Bi.Neema Daniel alimuahidi Bi.Sihaba kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa pamoja na kuiomba serikali kuwashika mkono hasa katika kurekebisha miundombinu ya shule hiyo ikiwamo mabweni na uzio wa shule. 

Naye Mhitimu katika mahafali hayo Rose Bryton amewataka wazazi na walezi kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwalinda watoto ili kuwawezesha kutimiza ndoto na matarajio yao kielimu. 

Akitoa ushauri kwa wazazi wenzake Bi Rebecca Peter amewataka wazazi kuachana na mila zilizopitwa na wakati za kuwaozesha watoto wa kike katika umri usiotakiwa kisheria bali kuwaendeleza kufikia ndoto zao. 

Jumla ya wanafunzi 143 wamehitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama

No comments: