Mwakilishi wa chama cha wamiliki na wauza mafuta rejareja Kanda ya kaskazini Deipyen Bameda (kulia) (TASDOA ) katikati ni Katibu mkuu TASDOA Tinno Mmasi akiwa anafafanua jambo mara baada ya kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Rambirambi zao za ifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent
Mkurugenzi wa Dar es salaam Independent School (DIS) Anna Msangi akiwa anakabidhi kiasi cha shilingi milioni tatu kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ikiwa ni mchango wao kwa wanafunzi wa Lucky Vicent
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiongea wakati wa kupokea rambirambi za wanafunzi 32 wa Lucky Vicent zilizotolewa na chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja na uongozi wa shule binafsi ya Dar es salaam Independent School (DIS)
Habari picha
na
Woinde Shizza, Arusha
Woinde Shizza, Arusha
Wanasiasa
wametakiwa kuacha mara moja kuchulia
tukio la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kama sehemu ya
kujinufaisha kisiasa, pamoja na baadhi yao kupotosha jamii
kupitia mitandao ya kijamii, amebainisha Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
Akipokea rambirambi za wanafunzi 32 wa Lucky Vicentzilizotolewa na chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja na uongozi wa shule binafsi ya Dar es salaame salaam Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea umaarufu.
Akipokea rambirambi za wanafunzi 32 wa Lucky Vicentzilizotolewa na chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja (TASDOA) pamoja na uongozi wa shule binafsi ya Dar es salaame salaam Independent School (DIS) ambapo alisema kuwa anasikitishwa sana na baadhi ya viongozi kuchukulia swala hili kama ni sehemu ya kujijengea umaarufu.
Alisema kuwa
swala hili sio tukio la kisiasa bali ni mtihani
na changamoto kubwa iliyozikumba familia za wananchi wa Arusha ,hivyo
linatakiwa kuheshimika na kuchukuliwa kama ni tatizo kubwa lililowakumba
wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kwani kuwapoteza watoto hawa
ni jambo la kusikitisha sana kwani walikuwa
wanategemewa kuwa viongozi wa baadae.
“Pia napenda
kuchukuaa fursa hii kuwashukuru kwa kuleta
michango yenu kwa ajili ya wanafunzi hawa 32 ila napenda pia kuwakumbusha
kuwa jumla ya watu wote waliopata tatizo
walikuwa 38 lakini kati yao waliokufa ni 35 na
na wingine watatu ni majeruhi hivyo napenda kuwasihi wananchi na
mashirika ambayo wanaleta msaada wasiangalie waliopoteza maisha tu bali
wawakumbuke na wale majeruhi watatu ambao wapo nje kwa matibabu kwani wao pia
ni binadamu”alisema Gambo
Alisema kuwa
japo kuwa majeruhi wale waliopelekwa nje
kutibiwa wanaudumiwa bure lakini kuna wale watu ambao wameenda nao pamoja ya
kuwa wanahudumiwa chakula na malazi lakini kwa binadamu waka waida anatakiwa
kujitegemea kwa vitu vidogovidogo hivyo ni vizuri kama watu wanaotoa msaada
wata wakumbuka na hawa majeruhi.
Kwa upande
wake katibu mkuu wa chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja
(TASDOA) Tino Mmasi alisema kuwa wao kama wamiliki wawauza mafuta wadogowadogo
wameguswa sana na msiba huu na ndio maana walioamua kukaa kama wanachama na
kuchanga fedha hizi kiasi cha shilingi millioni saba laki saba
ili ziwafariji wafiwa hawa 35 na pia wameaidi
kwend a kujichanga tena kwa ajili ya
kuwachangia majeruhi ambao wapo Marekani
“Tumetoa hiki
kidogo lakini kwa jinsi tulivyoguswa tutaenda kuchanga fedha
zingine
kwa ajili ya majeruhi waliopo marekani na tunapenda kukuaidi mkuu wa mkoa
tutakuwa nanyi bega kwa bega hadi majeruhi hawa wote wapone na warudi hapa
nchini”alisema Mmasi
Katika
michango hii shule ya
shule binafsi ya Dar es salaam Independent School (DIS) ilichanga kiasi
cha shilingi milioni tatu laki moja na nusu huku
chama cha wamiliki wauza mafuta rejareja
wakiwa wamechangia shilingi milioni saba laki saba huku wote
wakiahidi kwenda kukusanya fedha
nyingine kwa ajili ya majeruhi.
No comments:
Post a Comment