Monday, May 15, 2017

UJAZO WA LITA 6494 ZA DAWA HATARI ZAKUTWA KWENYE GHALA MWENGE

 Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge 
  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya athari za Dawa hizo ambazo zilikamatwa katika moja ya Maghala huko Mwenge 
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akitoa ufafanuzi  juu ya  kemikali bashirifu zinavyoweza kuchepushwa kwa matumizi mengine
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha baadhi ya Maghala kwa ndani sehemu ya ghala ya kuhifadhi Dawa.
Kamishna Msaidizi wa  Mamlaka ya Kupambana na Dawa Bertha Mamuya akionesha ghala la pili la kuhifadhi Dawa ambapo wamebaini kuwapo kwa dawa zilizomaliza muda wake.
Sehemu ya  nje ya jengo la kampuni ya  Tecno Net Scientific  ambalo lilitumika katika kutengenezea na kuhifadhi madawa hayo 

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini inamshikilia mmiliki wa kampuni ya Techno Net Scientific kwa kuingiza kemikali bashirifu nchini zenye ujazo wa lita 6494 kwa kukiuka sheria na taratibu.
 Imeelezwa kuwa, mmiliki huyo amekiuka sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya 2015 na ile usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani, sheria ambayo inasimamiwa na Mkemia mkuu wa Serikali..

Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na dawa za kulevya Rogers Sianga amesema kuwa, Kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni hiyo, yenye makazi yake eneo la mwenge kunatokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema mwezi uliopita waliowataarifu kuwa kampuni hiyo inaagiza kemikali bashirifu, ambazo ni hatari kwa matumizi na zisiporatibiwa zinaweza kutumika vibaya na kuleta madhara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, baada ya ziara fupi ya kutembelea maghala mawili ya kampuni  hiyo yanayotumika kuhifhadhia kemikali hizo, Sianga amesema, uchunguzi wao umeonyesha kuwa, kampuni hiyo inaagiza kemikali bila kibali.

“Tulichogundua ni kwamba kampuni hii ya Tecno Net Scientific yenye makazi yake eneo la mwenge, imeagiza kemikali nyingi ambazo ni bashirifu, kemikali bashirifu ni kemikali muhimu kwa utengenezaji wa kawaida wa dawa za binadamu lakini pia zikichepushwa  zikiwa diverted zinaweza kutengeneza dawa za kulevya za Heroine, Cocaine na nyinginezo ambazo huzalisha kemikali taka zenye sumu ambazo zinaweza kuhatarisha afya za watu na kuchafua mazingira.

Ameongeza kuwa,wamegundua kuwa kampuni hiyo pia iliagiza kemikali nchini ufaransa kwa kibali cha kughusi na imekua ikiendesha shughukli zake za biashara ya kuuza kemikali bila kibali, licha ya vibali vyake kuisha muda wake tokea mwaka jana.

 Ameongeza kuwa, mmiliki huyo anaendesha biashara ya kemikali bila ya kuwa na wataalamu kwani yeye binafsi ana elimu cheti cha huku mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anaelimu ya darasa la saba na baadae akajiendeleza Veta na kuwa fundi magari wakati kisheria ili uweze kuendesha biashara hiyo unatakiwa uwe na kuanzia diploma ya kemia na kuendelea.

“Pamoja na Kemikali hizi bashirifu kuwa na matumizi halali kama viwandani na hospitali lakini zimewekewa utaratibu wa udhibiti kitaifa kitaifa na kimataifa kuanzia ununuaji, usafirishaji, jinsi ua uhifadhi na utumiaji wake kwakuwa kemikali hizo zikiachwa bila udhibiti watu wenye dhamira mbaya wanaweza kuzitumia kutengeneza dawa za kelevya”, amesema Sianga.

Ameongeza kuwa mamlaka inachunguza tuhuma dhidi ya kampuni hiyo zikiwezo za kumiliki kemikali ambazo hazijasajiiwa na mamlaka husika kinyume na sheria baada ya usajili wake katika biashara kukoma, kutokuwa na taarifa za mwenendo mzina wa kemikali wanazoingiza  nchini na kuzisambaza kwa wateja, na nyinginezo nyongo.
Amesema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea na utakapokamilika hatua za kesheria zitachukuliwa na atafikishwa mahakamani.
Mwisho

No comments: