Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni
ya Saruji nchini ya Tanzania Portland Cement inayozalisha Twiga Cement,
imesema kuwa itaendelea kuwa kinara kwa mauzo ya Saruji hapa nchini,
licha ya kuwepo wa viwanda vingi katika miaka ya hivi karibuni.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alfonso Velez, alipokuwa akitoa
ripoti ya mauzo ya kampuni hiyo na changamoto inazokabiliana nazo
katika mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo.
“licha
ya makampuni mengine kuja na mpango wa ujanja wa kushusha gharama za
saruji bado Twiga Cement imeendelea kuwa ndio saruji bora kwenye soko
licha ya changamoto ya kupambana na bei ya soko”
Amesema
wao wameshuhudia wakiona washindani wao wakihangaika juu ya upataji wa
mali ghafi ambazo zitaweza kuwasaidia kuendelea kufanya bishara kwa bei
ya chini lakini TPCC bado haijatetereka.
Amesema
kuwa mshindani wake bado ana wakati mgumu kwani yuko mbali na soko na
inamchukua muda mrefu kusafirisha mzigo mpaka sokoni hivyo wakati wowote
atapandisha bei ya saruji na Twiga itabaki pale pale, kwani ameweza
kufanya hivyo katika nchi zingine alizowekeza ambapo amepandisha bei
kuwa juu hili kufidia gharama za uzalishaji.
Mwenyekiti
wa bodi ya kampuni ya TPCC , Osward Urasa akizungumza katika mkutano
huo juu ya wanahisa kutoa taharifa zitakazosidia kujenga kampuni kuzidi
kuwa imara.
Mwenyekiti
wa kampuni ya Tanzania Portland Cement, Alfonso Rodriguez akizungumza
katika mkutano huo wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo katika
hotel ya Ramada
Mkaguzi
wa Mahesabu wa kampuni hiyo kutoka kampuni ya Ernist nd Young ,
Elibariki Fanuel akieleza juuya mehesabu ya mwaka ya kampuni hiyo
Mkurugenzi
wa Twiga Cement Alfonso Velez akizungumza juuya mafanikio ya kampuni
hiyo mara baada ya kuwepo wa ushindani wa makampuni mengine nchini
Sehemu ya Wanahisa katika mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa makini
Profesa akijadili jambo na wakurugenzina uongozi wa juu wa Twiga Cement
Katibu wa kampuni TPCC,Brain Kangeta akizungumza wakati wa mkutano huo wa wanahisa na wateja wa Twiga Cement
Mwanahisa Christopher Mvemo akichangia jambo juu ya kuboresha kampuni hiyo ili izidi kuwa kinara wa mauzo ya Saruji
Mwana hisa , Godfrey Marik akiuliza swali juu ya mipango ya kampuni katika kuhimili ushindani na makampuni mengine
sehemu ya wajumbe wa mkutano huo waliohudhuria
No comments:
Post a Comment