Wednesday, May 3, 2017

TUPO TAYARI KULIPA FIFA DOLA 15,000 ILI KUPATA HAKI- AVEVA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa Klabu ya Simba, umeweka bayana uamuzi wao wa kwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kudai haki yao baada ya kupokwa pointi tatu na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji huku wakiwa wanasubiri barua kutoka Bodi ya Ligi ili wawasilishe malalamiko yao.

Simba imefikia hatua hiyo baada ya Kamati ya utendaji kukaa na kuamua kwa kauli moja kulipeleka mbele zaidi suala hilo kutokana na kuona kasoro za kikanuni katika maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Usimamizi wa Ligi kwa sababu ambazo wanaziona si za msingi kutokana na kanuni kuwa wazi.

Akizugumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam, Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, amesema wanachokisubiria kwa sasa ni ku njia zipo nyingi za wao kupata haki yao, hivyo wanasubiri kupewa barua kutoka Bodi ya Ligi ambayo wataiambatanisha kwenda Fifa kudai haki yao.

Aveva amesema wamefuatilia njia za kudai haki yaona wameambiwa gharama inaweza kuanzia dola 15,000 na wapo tayari kulipa ili tupate haki yao ambayo mpaka sasa wanasikia tu kama wamepokwa pointi 3 walizopatiwa na kamati ya saa 72 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar ambayo inadaiwa ilimchezesha beki wake, Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano dhidi yao.

Maazimio hayo yaliyofikiwa kwa pamoja na kamati ya utendaji yameainisha kuwa pamoja na hilo, pia wanapeleka malalamiko yao kuhusiana na mchezaji wao Mbaraka Yusuph aliyeidhinishwa kucheza katika klabu ya Kagera wakati tayari akiwa na leseni ya kuchezea ya klabu ya Simkba.

"tunafahamu kuwa TFF wanakuwa ni wazito katika kusikiliza masuala au malalamiko ya klabu yetu ya Simba, tukianzia na kesi ya Singano, mchezaji Mbaraka Yusuph ambaye anacheza Kagera kwa sasa wakati wao kama Shirikisho walitoa leseni ya mchezaji huyo kwetu sisi na kila kitu kipo wazi kabisa,"amesema Aveva.

Mbali na hilo, Aveva uamuzi wa Rais wa TFF kupeleka fainali Jamhuri Dodoma wala hatuwezi kuupinga kwani Simba imejiandaa kucheza fainali sehemu yoyote kwani hakuna wa kuizuia pale inapotaka jambo lake.

Aveva ametoa kauli hiyo baada ya jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa rais wake, Jamal Malinzi kutangaza mechi ya fainali ya FA kati ya Simba na Mbao itapigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

"sisi hatuidharau Mbao, ila hatuiogopi kwani ni timu ndogo na hata katika mkoa wa Dodoma tuna mashabiki wengi sana tunachotaka kuwaambia kuwa fainali tutacheza kokote,"amesema Aveva.


Raisi wa Klabu ya Simba Evance Aveva akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uamuzi wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kuazimia kwa pamoja kupeleka malalamiko yao Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kutokana na kutokufa nyiwa haki na Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini TFF.
 Raisi wa Klabu ya Simba Evance Aveva akionesha leseni ya mchezaji Mbaraka Yusuph waliyopatiwa na  Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini TFF,

No comments: