Tuesday, May 16, 2017

TRADEMARK EAST AFRICA, YAIWEZESHA ZANZIBAR KUONGEZA UFANISI WA KIBIASHARA KWA KUTUMIA MFOMO WA SMS KUSAJILI CHETI CHA UHALISI, NA KURIPOTI VIKWAZO VYA KIBIASHARA.

• Mradi unafanywa kwa ushirikiano kati ya TradeMark East Africa, (TMEA), TCCIA na ZNCCIA. mradi ulioanzishwa mwaka 2012 kwa TCCIA na kisha kupanuliwa kwa ZNCCIA mwaka, 2016.

• TMEA  imetumia zaidi ya Dola za Marekani,  $ 600,000 katika mradi huu wa (TCCIA & ZNCCIA).
• TMEA imegharimia gharama zote, ambapo, ZNCCIA imefaidika kwa kupatiwa vifaa vya ICT vyav kutekeleza mfumo, vifaa vya nishati ya jua kama nishati mbadala umeme unapokatika, na mshauri elekezi  kuratibu mradi huo na misaada ya kiufundi kuendesha.
Zanzibar, Tanzania, Mei 16, 2017 - Zanzibar inatarajiwa kunufaika na kufaidika na mfumo madhubuti na wa kisasa wa usajili vyeti vya uhalisia (certificate of orgin) na kuripoti vikwazo vya kibiashara kwa kutumia SMS za simu za mkononi, baada ya uzinduzi wa mfumo wa ufuatiliaji wa vikwazo visivyo kwa kiforodha, (NTB) na usajili wa vyeti  vya uhalisi uliofanywa kwa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Zanzibar, (ZNCCIA) kwa ufadhili wa taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA).
Mifumo hii miwili itasisimua zaidi maendeleo ya biashara Zanzibar, kama sehemu ya juhudi za Zanzibar kuiwezesha sekta binafsi  kufanya biashara kwa urais zaidi, kwa ufanisi kwa kuleta tija.
 Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Ali Bakari Ali, Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCCIA, Bi Munira Humoud na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA nchini Tanzania, John Ulanga.
Mifumo hii miwili itasaidia Zanzibar, kupitia ZNCCIA kuboresha mazingira ya kufanya biashara Zanzibar kwa kupata taarifa za vikwazo vya kibiashara, NTB, kwa haraka na  kwa uhakika, na kuzifikisha kunako husika kwa ufuatiliaji zaidi. taarifa zilizokusanywa na msaada wa mfumo NTB. Utoaji cheti cha uasili kwa njia ya mtandao, utapunguza muda wa upatikanaji  wa vyeti vya asili kwa kupunguza muda wa ufuatiliaji wa  hati hizo. Lengo ni kupunguza muda kwa ajili ya utoaji wa vyeti hivyo vya uasili kutoka siku nne za sasa, hadi siku moja tuu tena kwa saa chache.
Baada ya mfumo kama huu kutumiwa na Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania, TCCIA, vyeti zaidi ya 1000 vya uasili zimetolewa kielektroniki na zaidi ya vikwazo 90 (NTBs) kutatuliwa kwa upande wa  sekta binafsi. Zaidi ya SMS 2000 zimepokelewa katika mfumo huo, wa kuripoti, NTB kwa kutumia SMS.
Fedha za kugharimia mpango huu, zimetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la kimataifa,  (DFID) kupitia TradeMark, East Africa, (TMEA) inayosimamia utekelezaji wa  mradi huo.Mgeni rasmi katika uzinduzi, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Ali Bakari Ali,  alisema, "Serikali ya Zanzibar anaishukuru TMEA kwa  msaada huu muhimu ambayo inatarajiwa kuongeza ufanisi wa biashara na kuboresha biashara ya ushindani wa Zanzibar." 
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, "Sisi kama TMEA tuna furaha kubwa kusaidia mifumo hii miwili kufanya kazi kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Zanzibar,hivyo kukuza biashara  na kuleta ufanisi wa biashara ya Zanzibar yenyewe kama Zanzibar, Zanzibar na Tanzania Bara, na Zanzibar nan chi nyingine”.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCCIA, Ms.Munira Humoud amesema, "Tunaishukuru TMEA kwa misaada hii,  kwa ZNNCIA ambapo mifumo hii mawili muhimu itaongeza ushindani visiwa Zanzibar kwenye biashara ya kimataifa kwa kuongeza kasi ya usajili wa vyetu vya uasili na kupunguza vikwazo vya kibiashara, NTBs kufuatia vikwazo hivyo kushughulikiwa mapema baada ya taarifa kupokelewa kupitisa SMS.


No comments: