Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari 2017 linalofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua moja ya semina za
mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani
ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
KILA ifikapo
Mei 3 ya kila mwaka wanahabari na wadau wa vyombo vya habari
ulimwenguni huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Maadhimisho ya mwaka huu (2017) kitaifa nchini Tanzania yalifanyika
mkoani Mwanza na kushirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa
vyombo vya habari.
Miongoni
mwa hoja zilizoteka mijadala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2017 jijini Mwanza ni suala zima la
usalama wa wanahabari wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao pamoja na uwepo
wa mafunzo anuai ya mara kwa mara kwa wanahabari kuwanoa zaidi.
Chama
cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), ni miongoni mwa taasisi wadau
waliofanikisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani mwaka 2017 kitaifa yaliofanyika mkoani Mwanza. Bi. Valerie Msoka
ni Mwanachama wa TAMWA, akizungumza katika maadhimisho ya mwaka huu
kuwasilisha ujumbe wa chama hicho kwa wadau wa habari.
Anasema
TAMWA imejitahidi katika kuwanoa wanahabari ili kuhakikisha wanabobea
kwenye maeneo mbalimbali ya uandishi wa habari huku lengo likiwa
kuwajengea uwezo zaidi. Bi. Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA hapo nyuma kabla ya uongoziwa wa Mkurugenzi wa sasa wa
chama hicho, Edda Sanga anabainisha wamekuwa mstari wa mbele katika
kuchangia weledi na ubobezi wa wanahabari hasa katika uandishi wa habari
za ukatili kwa jamii.
Anasema
tamwa katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kwa kipindi
cha mwaka 2015 na 2016 imeelimisha idadi kubwa ya wanahabari kwenye
ubobezi wa uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia eneo ambalo
limekuwa likionekana kupwaya kiuandishi.
Wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2350 na
wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsia ya kuandika habari za ukatili
wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo
hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali.
Anasema
waandishi hao baada ya kupata mafunzo hayo wamekuwa wakitumia ujuzi huo
kuandika na kuibua habari za vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo
ambalo limesaidia baadhi ya maeneo mamlaka husika kuchukua hatua juu ya
vitendo hivyo, hali ambayo imekuwa ikisaidia kupungua kiasi fulani kwa
vitendo hivyo kwenye jamii ukilinganisha na hapo awali. Baadhi
ya wanahabari wapiga picha ambao walishiriki mafunzo ya upigaji picha
za ukatili yaliyoandaliwa na TAMWA wakimsikiliza mkufunzi wa mafunzo
hayo, Mwanzo L. Millinga (wa kwanza kulia) kutoka ‘Practical School of
Journalism’ (PSJ). Mratibu
wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kulia)
akizungumza katika moja ya mikutano ya mafunzo kwa wanahabari na wadau
mbalimbali wa TAMWA.
Aidha Bi. Msoka anaongeza kuwa
utaratibu huo wa kuwajengea uwezo wanahabari umekuwa ukifanywa mikoa
mbalimbali huku ukijumuisha wanahabari kuandaliwa kimafunzo katika
semina kadhaa na baadaye kufuatiliwa kwenye utendaji ili kubaini
mabadiliko kimafanikio kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo waliyopata.
Wananchi
kwa upande mmoja nao wamekuwa wakihamasika na kutumia vyombo vya habari
katika kuibua matukio hayo ya kikatili, jambo ambalo limeanza kuleta
mafanikio kiasi fulani. Bi. Msoka anaendelea kubainisha kuwa TAMWA
katika kutekeleza mradi wake wa GEWE II kimeweza kuunda kamati za
kuelimisha jamii jinsi ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia
katika wilaya kumi za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, ambazo
zinawahusisha wanahabari ili kuwezesha jamii kushirikiana na vyombo vya
habari kuweza kuvitolea taarifa vitendo hivyo bila woga. Anaeleza kuwa
kwa kisi kikubwa kamati hizo zimesaidia kuibua matukio hayo kwa kiasi
kikubwa kwa vyombo vya habari.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome
Kitomari akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Pamoja
na hayo Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kinaamini kuwa kupitia
maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ya mwaka huu
(2017) wanahabari kwa kutumia changamoto zilizoibuka dhidi yao, katika
kujitathmini, watafanya kazi zao kwa weledi na uaminifu ikiwa ni pamoja
habari zenye usawa wa pande zote husika.
Hii
ni pamoja kujitahidi wanatasnia hiyo kuibua mambo yanayoweza kukwamisha
jitihada za maendeleo ili yafanyiwe kazi, pia kujiepusha na habari
ambazo kwa sehemu zinaweza kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao
wenyewe au wananchi katika taifa la Tanzania. Kama hiyo haitoshi TAMWA,
imeendelea kuwanoa wanahabari katika nyanja nyingine za kimafunzo. TAMWA
ilijiunga katika mapambano ya ajali za barabarani kwa kutoa mafunzo kwa
wanahabari mbalimbali.
Katika
ufafanuzi juu ya hatua hiyo inabainisha kuwa ajali za barabarani
zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga anasema katika moja ya mafunzo kwa
wanahbari kuwa wana kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali
nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi
kikubwa. Anasema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na
kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto
pasipo na msaada kwa kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika
familia. Sehemu
ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa
katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam Sehemu
ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa
katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment