Saturday, May 6, 2017

SINGIDA INAZALISHA NUSU YA ASALI YOTE INAYOZALISHWA NCHINI; WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AELEZA.

 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha wazalishaji nyuki cha Kisaki katika manispaa ya Singida.

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali inayozalishwa na kikundi cha wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kikundi hicho Philemon Kiemi. 


Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward Mashimba kwa kuhitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya kumtunuku cheti cha mafunzo hayo.
Eneo la kikundi cha wafugaji nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya kutosha katika kijiji cha Kisaki, Manispaa ya Singida. Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha uzalishaji nyuki Philemon Kiemi.

……………………………………………………………………………….

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda Mkoa wa Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.

Amesema Singida imekuwa ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi nzima ukiwa ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.

Mheshimiwa Pinda amesema asali ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana pia dawa huku akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta kuzalisha mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata soko la ndani.

Ameongeza kuwa kuwa wananchi watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta milioni 35 kufuga nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku ikiwafaidisha kwa kuvuna asali na mazao yake.

Mheshimiwa Pinda amewaasa vijana waliohitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kuhakikisha wanaisambaza elimu waliyoipata kwa wenzao pamoja na wao kuwa wagujai nyuki wa mfano katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singda Elias Tarimo amesema Manispaa ya Singida ina vikundi 16 vya uufugaji nyuki na wafugaji nyuki wengi wakiwa katika kata za Uhamaka, Mungumaji, Mtamaa, Mwankonko na Kisaki.

Tarimo amesema wataendelea kuhamasisha vijana na wakazi wengi kufuga nyuki kisasa na kusisitiza ufugaji nyuki kibiashara ndio wenye tija na manufaa kwa mfugaji.

Mmoja wa wahitimu Jacob Edward Mashimba amesema mafunzo ni mazuri na yatawasaidia katika kutunza mazingira kutokana na jamii imekuwa ikikata miti kwa wingi.

Mashimba amesema katika jamii anayotoka ya kihadzabe ambayo bado inategemea asali kama chakula kikuu elimu ya ufugaji nyuki kibiashara itasaidia licha ya upungufu wa baadhi ya vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki.

No comments: