Sunday, May 14, 2017

SIMU TV:HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imewahakikishia watanzania kuwa dawa zinazoingizwa hapa nchini zimekidhi viwango vya ubora. https://youtu.be/P9Zreo51hiU

SIMU.TV: Jamii ya kifugaji hususani kabila la wamasai wameshauriwa kubadili mtazamo wa kujikita zaidi katika shughuli za maendeleo na kuchangia fedha katika miradi ya maendeleo inayoanzishwa na serikali. https://youtu.be/pJ7ZahrcrvA

SIMU.TV: Kiwanda cha kutengeneza mashine za viwandani KTMC Kilimanjaro kipo mbioni kupata mtaji wa shilingi bilioni 1.5 ili kurejesha shughuli zake za uzalishaji. https://youtu.be/UvXVx6oZFnU

SIMU.TV: Wakulima nchini wametakiwa kuingunga mkono serikali kwa kutumia njia za kisasa za kilimo ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda. https://youtu.be/jw4id2uBl-8

SIMU.TV: Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amour Ahmad Amour ametoa muda wa siku tatu kwa mhandisi wa maji katika halmashauri ya Masasi kukamilisha mradi wa maji uliokwama kwa zaidi ya miaka minne. https://youtu.be/z2VHtZHCsTs

SIMU.TV: Kampuni ya uchimbaji wa makaa ya mawe TANCOAL katika mgodi wa Ngaka mkoani Ruvuma imetekeleza agizo la waziri mkuu la kuongeza uzalishaji mara mbili zaidi. https://youtu.be/FvahNvKVgm0

SIMU.TV: Wafanyabishara na wasafirishaji wa ng’ombe katika mnada wa Pugu jijini Dar es Salaam wamelalamikiwa muda waliopewa kufanya shughuli zao katika eneo hilo kuwa hautoshi na unakwamisha biashara zao. https://youtu.be/KL3e1Q5OlDg

SIMU.TV: Kufuatia kutokamilika kwa miradi ya maji katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza serikali imeitaka kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza huduma hiyo kukamilisha miradi ya maji kwa wakati. https://youtu.be/URATz2zQ6qg

SIMU.TV: Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala ametoa wito kwa wahitimu wa kidato cha sita kuzingatia maadili mazuri waliyotoka nayo shule za sekondari wakati wakijiunga na vyuo vikuu. https://youtu.be/aDjjIUfKtZs

SIMU.TV: Wazazi wameaswa kufuatilia maendeleo ya watoto wao wakiwa shuleni pamoja na kushirikiana na waalimu ili kuwezesha watoto wao kupata elimu bora. https://youtu.be/YZk4uX3BItA

SIMU.TV: Rais wa shirikisho la riadha Tanzania Antony Mtaka amesema kuwa Tanzania itafanya vizuri katika michuano ya riadha kufuatia kupatikana kwa wachezaji wengi wenye viwango vya kimataifa. https://youtu.be/l-BeFJYvE9w

SIMU.TV: Mashindano ya ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam yameendelea tena leo ambapo timu ya Kurasini Divers ilichapwa na Oilas. https://youtu.be/0cMemXKItlY

SIMU.TV: Kukosekana kwa wadhamini na wadau wa kuunga mkono mpira wa miguu kwa timu za wanawake kumesababisha kuzorota kwa mchezo huo mkoani Manyara. https://youtu.be/Zq_CFq6HB5s

No comments: