Monday, May 22, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Watoto 100 watafanyiwa upasuaji wa moyo bure na madaktari bingwa kutoka India katika hospitali ya Regency jijini Dar Es salaam ; https://youtu.be/tJmPCWtDA8c

SIMU.TV: Idadi ya watu wanaotumia daraja jipya la Kigamboni imezidi kupungua siku hadi siku kutokana na uchakavu wa barabara za kufika katika daraja hilo; https://youtu.be/pOALVIAR_4I

SIMU.TV: Shirika la utangazaji TBC na Tanapa wameanza kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuanzisha channel mpya ya wanyama na kutangaza utalii nchini; https://youtu.be/USoW__gCpmQ

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu amekemea ubinafsi wa baadhi ya viongozi na kusababisha kuchelewa kwa shughuli za maendeleo; https://youtu.be/BlXVjMJIrms

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar Es salaam limekamata magari mabovu 119 ambayo yanatumika kubebea wanafunzi hivyo kuhatarisha usalama wao; https://youtu.be/TdKzua01yz8

SIMU.TV: Bei ya samaki katika soko la samaki la kimataifa la Feri imepanda maradufu kutokana na kuadimika kwa samaki; https://youtu.be/wVEmV3z73Do

SIMU.TV: Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dkt Kimei amesema ameshuka kwa faida kwenye benki hiyo kumesababishwa na kuondolewa kwa fedha za umma kwenda BOT; https://youtu.be/-0iM1FvTtuU

SIMU.TV: Baadhi ya wakulima wa karafuu visiwani Zanzibar wamewalalakimia maafisa kilimo kwa kushindwa kuwatembelea mara kwa mara; https://youtu.be/I7yAUzYjY9A

SIMU.TV: Mashabiki wa soka nchini Tanzania wamepokea kwa hisia tofauti taarifa za kutolewa kwenye mashindano ya vijana timu ya Serengeti boys; https://youtu.be/FApVe3V4uMI

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuwekeza kwenye soka la vijana ili kuleta maendeleo ya soka kwa watanzania; https://youtu.be/VK9T2i6P9Ms

SIMU.TV: Watanzania wametakiwa kuziandaa vyema timu zao ili kuweza kufanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya  Standard Chartered; https://youtu.be/1Qnj3J_86V8

SIMU.TV: Mmiliki mwenye hisa nyingi  kwenye klabu ya Arsenal Stan Kraonke amesema kuwa hajawahi kufikiria kuziuza hisa zake hata siku moja; https://youtu.be/ITXj_tFET1g

SIMU.TV: Tanzania kesho inatarajiwa kuungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya Fistula huku serikali ikisisitiza kutolewa  kwa matibabu bure kwa akina mama wenye tatizo la fistula. https://youtu.be/bKl1HGudCwA

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wanne katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/Ov2OHTKLwac

SIMU.TV: Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeitaka serikali kupitia jeshi la polisi kutumia njia mbadala ya kubaini chanzo na wahusika wa mauaji ya raia katika maeneo ya mkoa wa Pwani. https://youtu.be/BGS0K8oWr-s

SIMU.TV: Wananchi wameombwa kushirikiana na shirika la viwango TBS kwa kuhakikisha vifaa wanavyotumia katika ujenzi vinakidhi ubora unaotakiwa. https://youtu.be/WYndKx_-z-8

SIMU.TV: Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Dr. Cherles Kimei amesema kuhamishwa kwa amana za mashirika ya umma kwenda benki kuu kumeathiri biashara katika sekta ya benki nchini. https://youtu.be/45_c0nhdJ9s

SIMU.TV: Takribani watanzania milioni 50 wanahitaji huduma za wabunifu na wakadiriaji majenzi huku idadi ya wataalamu waliosajiliwa katika taaluma hiyo haifiki elfu moja. https://youtu.be/RGg-4l7HVoY

SIMU.TV: Wakazi zaidi ya elfu nane wa mtaa wa Amani manispaa ya Temeke wamekumbwa na kadhia ya kuharibika kwa kituo cha daladala kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. https://youtu.be/x_9BFC9_Yv0

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imetangaza msamaha wa kodi ya majengo kwa wazee waliostaafu, wenye ulemavu pamoja na wazee wasiojiweza. https://youtu.be/YgUYA5VNZvA

SIMU.TV: Wakazi wa mkoa wa Mtwara wameanza kunufaika na ajira za viwandani baada ya serikali kuwataka wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho mkoani humo kuvifufua viwanda hivyo. https://youtu.be/8flDvEhMTj4

SIMU.TV: Baraza la sanaa la taifa BASATA limesema limeshangazwa na taarifa za kusambaa kwa picha za utupu za mwanamuziki Benard Paul na linafanya utaratibu wa kumhoji ili kujua undani wa tukio hilo. https://youtu.be/Uw79wMuJk5E

SIMU.TV: Mbunge wa jimbo la Singida mjini Musa Sima amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Singida. https://youtu.be/rYAP07YGttw

SIMU.TV: Timu ya soka ya Azania imeondolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Standard Chartered inayofanyika huko nchini Uingereza. https://youtu.be/-lfJFY1-g2w

No comments: