Monday, May 8, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu ameongoza maelfu ya waombolezaji mkoani Arusha kushuhudia kuagwa kwa miili ya wanafunzi waliofariki kwenye ajali; https://youtu.be/GU2btUFIy3g

SIMU.TV: Jumuiya ya wanafunzi wa shule za msingi kata ya Kawe wameungana na kuwaombea wanafunzi wenzao walipoteza maisha mkoani Arusha; https://youtu.be/sIr-KwQutaw

SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajia kuwasili nchini Tanzania siku ya Jumatano kwa ajili ya ziara ya kikazi; https://youtu.be/JWtmRfiX4Bo

SIMU.TV: Benki kuu ya Tanzania BOT imeifutia leseni ya biashara benki ya kimataifa ya FBME na kuiweka chini ya Ufilisi; https://youtu.be/moQe7oXU2RY

SIMU.TV: Serikali nchini Tanzania imekiri kuwepo kwa changamoto za usawa katika viwango vya ubora wa elimu ya juu kwa nchi wanachama wa Afrika mashariki; https://youtu.be/tAtcYeQV26s  

SIMU.TV: Wananchi wengi wilayani Chunya mkoani Mbeya wanaogopa kujiunga kwenye vyama vya ushirika kutokana na kugubikwa na ubadhirifu wa fedha; https://youtu.be/0VMvnRIsgfA

SIMU.TV: Kampuni ya utengenezaji wa saruji ya Tanga Cement imetangaza mikakati yake ya kuendelea kuzalisha saruji yenye ubora zaidi; https://youtu.be/MxGjf_Oihe0

SIMU.TV: Asasi za kifedha zimetakiwa kuunga mkono jitihada za serikali kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kuwakopesha mikopo nafuu watanzania; https://youtu.be/0jXV9kNm8F4  

SIMU.TV: Wachezaji wa klabu ya Ndanda Fc wamesema hawatoweza kusafiri kwenda mkoani Mbeya kucheza na Tanzania Prisons mpaka walipwe mishahara yao; https://youtu.be/RAXDoARD7tY

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu TFF limeendelea kuwaomba wadau wa michezo nchini kuendelea kuwachangia Serengeti Boys; https://youtu.be/9OifPfA6ZEo

SIMU.TV: Msanii Mrisho Mpoto amesema Tanzania imepata msiba mkubwa ambao ni vigumu kusahau hivyo ameamua kutunga wimbo wa kuomboleza; https://youtu.be/DD8VXAaAqVo

SIMU.TV: Furahia habari motomoto za soka kunako anga la kimataifa ambazo tumefanikiwa kukukusanyia kwa siku ya leo; https://youtu.be/2k2ab1mAP0A

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amewataka madereva kuwa makini wawapo barabarani ili kuepusha ajali zinazopoteza maisha ya watu. https://youtu.be/WZ9ZgT-jvMc

SIMU.TV: Mwenyekiti wa chipukizi taifa wa chama cha mapinduzi CCM amewataka watoto nchini kutovunjika moyo na kusoma kwa bidii kufuatia vifo vya wanafunzi 33 wa shule ya Luck Vicent mkoani Arusha. https://youtu.be/Vo4G0r3x9EE

SIMU.TV: Serikali imeandaa nafasi za ajira elfu kumi na tano ili kufidia pengo la watumishi kwenye sekta mbalimbali za umma kufuatia kuondolewa kwa watumishi wenye vyeti bandia. https://youtu.be/qTKm8roxxMM

SIMU.TV: Mwenyekiti wa umoja wa vijana Afrika  hapa nchini James Magumba ameiomba serikali kuunda baraza la umoja wa vijana la taifa ili lisaidie kuleta maendeleo kwa vijana. https://youtu.be/mJj6wfALsEU

SIMU.TV: Timu ya madaktari bingwa kutoka nchini China imewasili mkoani Mara ambapo itatoa huduma za matibabu bure kwa wananchi wa wilaya ya Musoma vijijini. https://youtu.be/6jdbbpui0ww

SIMU.TV: Madiwani wa halamashauri ya wilaya ya Magu Mkoani Mwanza wameiomba serikali kusambaza dawa za kuulia wadudu wanao shambulia mazao ya chakula wilayani humo. https://youtu.be/_6ELQXsIaTI

SIMU.TV: Wakazi mkoa wa Kusini Unguja wametakiwa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa badala yake watumie nishati ya gesi ili kulinda mazingira. https://youtu.be/qgdaIgn_oIY

SIMU.TV: Wakazi wa manispaa ya Dodoma wameshauriwa kupima afya zao mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza. https://youtu.be/0N-QhiJ7UjI

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Nkasi amewataka askari wa kikosi cha kupambana na ujangili kuwa waadilifu ili kulinda upotevu wa rasilimali za nchi. https://youtu.be/ukYtqtPWV7g

No comments: