Wednesday, May 3, 2017

SHIRIKA LA ANGA ETIHAD LAMTEUA GAVIN HALLIDAY KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALA GROUP

Shirika la Anga la Etihad (EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji wake na kuimarisha huduma zake ulimwenguni.

Halliday ataliongoza shirika hilo katika kuendana na huduma bora ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kuwasogeza karibu wateja na kuendelea kufurahia huduma bora zinazotolewa na shirika hili pamoja na washirika wake wa ndege. Pia, atawajibika kuwa karibu na wabia wa EAG pamoja na kushiriki vikao vya utawala ambavyo ni ndiyo nguzo muhimu kwa mipango na maendeleo ukuaji wa biashara ya usafirishaji Abu Dhab na Nchi za Falme za Kiarabu.

Halliday anaungana na Shirika la Anga la Etihad baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa akifanya kazi kwa miaka 30 katika Shirika la Ndege la Etihad na kwenye Shirika la IAG. Kwa miaka mitatu ya hivi karibuni amekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Avios, ambayo ni programu maarufu ulimwenguni. Pia amewahi kuwa katika nafasi ya juu akihusika na masuala ya biashara kwenye Shirika la IAG, Iberia, British Midland na British Airways.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, H.E Mohomed Mubarak Fadhel Al Mazrouei alisema, “Hala ni nembo muhimu kwa Etihad ambayo imekuwa ikihakikisha inawaunganisha wabia wetu kwenye biashara ya usafiri wa anga. Pia ni idara muhimu ambayo imekuwa kiungo muhimu kwa wasafiri wa Abu Dhab na Nchi za Famlme za Kiarabu kwenye biashara na usafirishaji wa uhakika. Gavinni ni miongoni mwa watu muhimu kwenye sekta hii ya usafiri wa anga, hivyo tunafurahia kujiunga na timu ya uongozi wa EAG.

“Tumefurahishwa na uzoefu wa Gavin na tunaamini ataendeleza programu za masoko ulimwenguni jambo ambalo ndiyo mpango wetu mkubwa.”

Halliday alisema, “Hii ni nafasi ya heshima niliyoteuliwa. Shirika la Ndege la  Etihad ni miongoni mwa makampuni yanayokuwa kwa kasi kwenye sekta ya  anga katika karne hii. Hala ndiyo kitovu cha ukuaji huo. Ninatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na mashirika ya ndani ya usafirishaji na kupanua biashara na kuwavutia wasafiri wengi Abu Dhabi na Nchi za Falme za Kiarabu.”

Hala ilianzishwa mwaka 2016 ili kutekeleza mipango ya EAG ya kutoa huduma bora zaidi katika, usafirishaji na kibiashara. Hii inajumuisha Global Loyalty, Etihad Holidays, Hala Abu Dhabi, Hala Traveli Management na Amadeus Joint Venture.

Halliday ataanza rasmi majukumu yake mwezi Septemba mwaka huu.

Mabadiliko hayo, Halliday anachukua nafasi ya Darren Peisley ambaye kwa sasa ana kaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hala.

HE. Al Mazrouei alimshukuru Peisley kwa machango wake alioutoa akisema kwamba, “Darren amefanya mambo mengi mazuri akiwa Hala. Amekuwa mwanzilishi na kuimarisha biashara ya Global Loyality na kuitambulisha ulimwenguni ambapo hadi sasa inahudumia zaidi ya wananchama zaidi ya milioni 20.

Pia awali alipokuwa akiongoza idara ya biashara na aliwezesha kufanya mabadiliko kwa kipindi cha miaka saba akiwa na Shirika la Ndege la Etihad. Tunamshukuru kwa mchango wake na tunamtakia kila heri katika utendaji wake hapo baadaye atakaporudi Austaria.”
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group Gavin Halliday 
 

No comments: