Sunday, May 28, 2017

RIPOTI YA UNYWAJI WA MAZIWA NCHINI YATOLEWA KATIKA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYWAJI MAZIWA KITAIFA.


Na Abdullatif Yunus - Bukoba.
Wakati  Shirika la Afya Duniani  WHO na Shirika la chakula na Kilimo FAO likipendekeza kiwango cha unywaji maziwa kwa Binadamu ni  lita 200 kwa mwaka, imebainika kuwa nchi ya Tanzania unywaji wa maziwa  kwa mwaka ni asilimia 47, hii na sawa na chini ya robo ya kiwango kinachopendekezwa.

Kufuatia Ripoti hiyo iliyotolewa na Mh Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo Na Uvuvi Mhe. William ole Nashe (pichani) Serikali imejipanga kuboresha zao la maziwa kuanzia kwa Mfugaji mpaka kwa mtumiaji, ili kuhakikisha zao hili linakuwa na Tija,
Akihutubia katika Uzinduzi wa wiki ya  Unywaji  Maziwa Kitaifa inayoadhimishwa Mkoani  Kagera katika Manispaa ya Bukoba, Mh. Naibu Waziri Ole Nasha amesema,
“Takwimu Ya zao la maziwa nchini zinaonyesha kuwa,Nchi ya Tanzania huzalisha maziwa lita bilioni 2.1 kwa mwaka, ambapo 70% huzalishwa na Ng,ombe wa asili ambao uzalishaji wake ni kati ya lita mpaka lita tano kwa siku, hata hivyo tunao ng,ombe wachache wa maziwa wanakadiriwa kufikia Ng,ombe laki saba na elfu themanini na mbili ambao wanakadiriwa huzalisha maziwa lita nane hadi ishirini kwa siku.”

Aidha Mh. Naibu waziri William Ole Nasha, ameongeza kuwa “ maziwa yanayoingia viwandani kusindikwa kati ya maziwa yanayozalishwa ni  3% tu!, hapa nchini kuna viwanda 75 vyenye uwezo wa kusindika  lita laki sita na Arobaini elfu kwa  siku, lakini kwa sasa viwanda vinavyosindika Maziwa ni  63 tu vyenye uwezo wa kusindika lita laki moja na elfu sitini na saba na sabini za Maziwa kwa siku.
 Hii ni sawa na wastani wa unywaji wa maziwa, ni takribani lita 47  kwa mwaka”

No comments: