· ATAKAYEKAMATWA TUMBAKU YAKE KUTAIFISHWA
Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa
tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji
unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi
hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza
tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao.
Marufuku
hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya
ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo
kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia Chama gani cha Msingi.
Mkuu
wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha
wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na
mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya
kuanza kwa masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii
(26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
Alisema
kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama
vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu
wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni tumbaku ya wakulima wadogo
wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao
na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao
wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao
na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku
hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.
Alisisitiza
kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa ,
hawezi kukubali watu wakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka
kuwanyonya wakulima wengine.
Kufuatia
hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Wilaya
kushirikiana na Watendaji ngazi za chini na kuwakamata wao na mizigo
yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima
anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika
na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi wa tumbaku wenye
vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.
Atoa
angalizo kwa vyombo vyote vinavyotumika kusafirisha tumbaku kutoka eneo
moja kwenda jingine kuhakikisha mzigo waliopakia katika magari
unavibali vyote baada ya ununuzi katika soko kupitia Chama cha Msingi
ili kuepuka usumbufu na kuchukuliwa hatua.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Wakurugenzi Watendaji,
Maafisa Ushirika,Wanasheria na Wawakilishi wa Benki za CRDB na NMB kukaa
meza moja na kuangalia uwezekano wa kuweka makubaliano ambayo
yatawahakikisha wakulima wote wa tumbaku ambao walilima kwa kutumia
pembejeo zao wasiathirike na makato ya madeni ya wakulima wanaodaiwa.
Alipendekeza
kuwepo na Akaunti mbili, moja ni ile inayomlinda mkulima wa
aliyejitegemea na nyingine ya wakulima ambao wanadaiwa ili kila mtu
apate haki kulingana na alivyojiandaa katika kilimo hicho.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa
hakuna atakayenyimwa haki yake kwa sababu ya watu wengine.
Hata
hivyo wadau hao wa tumbaku walisema hakuna haja ya kuwa na akaunti
mbili badala yake Benki zinaweza kuweka utaratibu mzuri wa utambuzi wa
mtu aliyelima kwa kujitegemea na kumpa fedha zake zote na wale
wanaodaiwa wakaendelea na utaratibu wanaoutumia.
Walisema
kuwa hatua itawasaidia wakulima waliojitegemea na kuamua kuuzia tumbaku
yao kupitia vyama vya msingi kupata haki yao bila kuchelewa kwa
kusubiri deni la Chama cha Msingi limalizike kwanza ndio walipwe.
Naye
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amesema kuwa baadhi ya
matatizo na migogoro katika zao la tumbaku yamesababishwa na maslahi
binafsi ya baadhi ya watumishi wakiwemo Maafisa Ugani, Maafisa Ushirika ,
Wafanyakazi wa Mabenki na watumishi wengine wanaojihusisha ununuzi usio
halali wa zao hilo na kilimo hicho.
Alisema
kuwa watumishi hao ndio wamekuwa wakichochea migogoro na wengine
kuwarubuni wakulima kwa kununua tumbaku yao kinyume cha utaratibu na
kuwafanya walaze madeni.
Dkt.
Ntara alisema kuwa ili zao hilo limsaidie mkulima ni vema wataalum
wakafanyakazi zao za utaalam kuliko kuwa washindani wa wakulima na
hivyo wakati kuanzisha migogoro kwa maslahi yao binafsi ili hatimaye
wakulima wakate tamaa na kuanza kuuza tumbaku katika masoko yasiyo
rasmi.
No comments:
Post a Comment