Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Singida wakifuatilia kikao cha baraza hilo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
Wilaya ya Singida Rashid Mandoa (katikati) akimsikiliza kwa makini Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia kwake) na kushoto kwake ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Eliya Digha.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi akitunuku cheti kwa mmoja wa madiwani waliohitimu mafunzo
ya jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa
maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
………………..
Mkurugenzi wa halmashauri ya
Wilaya ya Singida Rashid Mandoa ameagizwa kuhakikisha ofisi za
halmashauri hiyo zinahamia ndani ya eneo la halmashauri hiyo na kutoka
walipo sasa katika manispaa ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo jana wakati akikabithi vyeti kwa
madiwani wa halmashauri ya Singida walipohitimu mafunzo kuhusu jitihada
za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo
iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Dkt. Nchimbi amesema endapo
mkurugenzi atahamishia ofisi na watendaji katika halmashauri yake
watapata ubunifu wa kutatua shida na kero za wananchi na hivyo
kuiendeleza halmashauri.
“Ukikaa kwenye nyumba
inayovuja ndipo utapata akili na ubunifu wa kutatua changamoto hiyo,
ukiangaia wanufaika wa Tasaf wameweza kufanya mambo mazuri kwa pesa
kidog waliyonayo, mkurugenzi uige mfano huo, mhamie katika halmasahuri
yenu, wananchi hawafurahii kuwaona ninyi na watendaji wengine mkiishi
manispaa” amesisitiza Dkt. Nchimbi.
Ameongeza kuwa kusitasita kwao
kutohamia katika halmashauri yao kutasababisha halmasahuri hiyo
ikavunjwa na hivyo kukosa ajira kwa watumishi huku akiwaeleza madiwani
kuwa wataponzwa wa kukosa kura katika uchaguzi ujao kwani wananchi
wangependa kupata huduma kwa ukaribu.
Dkt. Nchimbi amesema kuhusu
makao makuu ya halmashauri hiyo baraza la madiwani litachagua makao
makuu yao huku akishauri wazingatie eneo ambalo litafaa kwakuwa
Halmashauri hiyo inapitiwa na miradi mbali mbali ya kitafa ikiwemo mradi
wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga na ujenzi wa kituo cha
jeshi.
Akizungumzia mafunzo waliyopea
amesema ana imani kuwa sasa mafunzo hayo yataleta matokeo mazuri ikiwa
ni pamoja na kuwa na lugha nzuri ya kuwasiliana na wananchi na kujisogea
pamoja na wananchi, huku akiwaasa wasitumie kauli za kuwakatisha tama
wananchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida
Elias Tarimo amesema mafunzo yatawasaidia madiwani kusimamia miradi
ikamilike na iwe na ubora unao takiwa huku akitarajia kuona wananchi
wakiibua na kukamilisha miradi ya maendeleo.
Tarimo ameongeza kuwa madiwani
wanapaswa kuhakikisha simu huu wa mavuno wananchi wanavuna na kuhifadhi
mazao yao vizuri pamoja na kuwaelimisha wayatumie vizuri ili wapate
fedha za kujiendeleza.
Kwa upande wao madiwani hao
wamesema mafunzo hayo yamekuwa msaada kwao kwa kuwaelimisha majukumu yao
na mipaka yao ili waweze kitekeleza kwa ufanisi uwakilishi wao wa
wananchi.
Wamesema wengi walikuwa
hawafahamu mipaka yao na hivyo kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu
huku wakieleza kuwa mafunzo yameimarisha ushirikiano baina yao na
watendaji tofauti na hapo awali.
No comments:
Post a Comment