Thursday, May 25, 2017

PROF NDALICHAKO AWATUNUKU WAHITIMU WA MAFUNZO YA WAKATI UJAO YALIYOENDESHWA NA ATE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako amewataka wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao kujiendeleza zaidi ili kuweza kutimiza ndoto zao pamoja na kuwapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa juhudi kubwa wanazozifanya.


Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) yaliweza kuhitimishwa leo kwa wahitimu 33 kutunukiwa vyeti na Waziri Prof Ndalichako.

Akizungumza kabla ya utoaji wa vyeti kwa wahitimu Prof Ndalichako alisema kuwa ana imani kubwa kuwa mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wakufunzi wao watayatumia vizuri zaidi ni kutaka kuwaona wakiwa wamefika mbali zaidi.

"Programu hii kwangu ni fursa kwenu na mafunzo haya mkiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi chetu Kijacho," amesema Prof Ndalichako.

Kwa upande wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mkurugenzi Dkt Aggrey Mlimuka alisema kuwa ATE kupitia mpango huo wameweza kutoa mafunzi kwa wafanyakazi wa kike 33 kutoka makampuni 17 nchini.

"Tumetoa elimu hii tukishirikiana na chuo cha Mafunzo ya Uongozi Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI) kwa wafanyakazi wa kike 33 kutika makampuni 17 ambayi yamefadhili mafunzo haya,"amesema Mlimuka.

Amesema na mchanganyiko huu wa wakufunzi umechochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya makampuni na mafunzo hayo hutoa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mahali pa kazina katika maisha yao kwa kushirikiana na ESAMI.

  Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali ya mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).

Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) na kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozitumia katika kuwainua wanawake kimaendeleo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar akizungumza na wahitimu kabla ya kupatiwa vyeti hivyo kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).
 Wakurugnezi kutoka mashirika na kampuni mbalimbali wakitoa ushuhuda wa  namna walivyoanza mpaka walipo sasa, anayezungumza wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Barclays Abdi Mohamed.
Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akiwa anatoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO), kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri (ATE) Almas Maige,  Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar.

Wahitimu wa  mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako.

No comments: