Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia)
akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya
hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba
vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla
ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba
vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini.
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi.
Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa
tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba
ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na
Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi.
Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya
mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.
Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele
ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye
thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na
sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga akitoa ufafanuzi mchache jinsi alivyokuwa anaufahamu Mfuko wa Pensheni PPF.
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni PPF kanda ya Kaskazini na Kati na wafanyakazi wa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakielekea wodini.
—
Serikali
imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa
vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa
nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta
ya afya hapa nchini.
Akielezea
furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu
Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab
Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika
hospitali mbalimbali hapa nchini.
Kwa
upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na
kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa
wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa
Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja
kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika
mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa
kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya
16 vya serikali nchini.
Sehemu
ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa
tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na
wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha.
Naye
meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema
kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari ‘WOTE SCHEME’ ambapo
aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili
kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya
elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi
wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba
na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment