Tuesday, May 30, 2017

MFUKO WA PPF WAENDELEA KUKABIDHI VIFAA TIBA

Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. 
 
Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. 
 
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12 nchini. 
 
Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla thamani ya Sh. 99,983,700/-. Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine nchi nzima.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akiongea na wafanyakazi na wananchi waliojitokeza katika halfa ya kupokea vifaa tiba ikiwemo vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama kutoka kwa Mfuko wa PPF katika kutekeleza sera yake ya uchangiaji na udhamini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-KISARAWE. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa akielezea machache juu ya changamoto zilizokuwa zikiikabili wilaya yake katika upande wa afya. Pembeni yake ni Naibu wa Waziri (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani. Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akimkabidhi vifaa tiba kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

Vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa PPF.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo (wa tano toka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF na wafanyakazi wa wilaya ya Kisarawe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile akitoa shukrani Mfuko wa PPF kwa kutoa vifaa tiba.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel (wa pili kulia) na Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku wakiwaandikisha mwanachama mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.

Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.

No comments: