Na Karama Kenyunko- blogu ya jamii.
Mkulima mmoja Samwel Nicodem Bwandu 38, amehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamani ya milioni 60.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akisoma Hukumu, huyo hakimu shahidi amesema kuwa, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka bila ya kuacha shaka kuwa kweli Bwandu alikutwa na meno ya tembo lakini haukuweza kuthibitisha kuwa alikuwa akijihusisha na biashara hiyo.
Hata hivyo, mahakama hiyo,imemuachia huru Kidamisi Kidarageda Kidiwami, Mkazi wa Iringa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake kuwa alihusika katika tuhuma hizo za meno ya tembo.
Watuhumiwa wote wawili, Bwandu na Kidawami walikuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kupatikana na nyara za serikali ambazo ni vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamank ya milioni 600 na Kijihusisha na nyara hizo zenye thamani ya milioni 900.
Hakimu Shahidi amesema, amezingatia ushahidi wote uliotolewa na upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa na kuridhika kwamba mshtakiwa Kidawami hakuhusika katika kutenda makosa hayo.
"Hakuna shahidi yeyote aliyefika mahakamani hapo na kuthibitisha kuwa mshtakiwa wa Kidawami alihusika na tuhuma hizo, isipokuwa shahidi namba tano ambaye nae alikuwa na ushahidi wa kusikia tu", amesema hakimu Shahidi"
Ameongeza kuwa, kwa upande wa mshtakiwa Bwandu upande wa mshtakiwa wa upande umeweza kuthibitisha bila shaka kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo kwani hata aliposachiwa alikuwa na nyara hizo.
Kabla ya kumsomea adhabu yake baada ya kipatikana na hatia, hakimu Shahidi aliuliza upande wa mashtaka kama alikuwa na kitu chochote cha kusema ambapo, Wakili wa serikali, Elia Athanas aliiomba mahakama itoe adhabu stahiki kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa jamii nzima kwani vitendo vilivyofanywa na mshtakiwa vinachafua taswira ya nchi kimataifa
Ameongeza adhabu hiyo siyo tu itakuwa fundisho bali itasaidi dunia nzima ijue Tanzania iko serious katika kutatua tatizo lanuharibifu wa maliasili na kuirudisha nchi katika hadi yake.Naye mshtakiwa Bwandu katika utetezi wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ameishakaa sana gerezani.
" Mahakama inakuhukumu kwenda jela miaka 20 na hapo nimezingatia na muda uliokaa gerezani lakini kwenye suala la faini lipo kisheria ambapo MTU anatakiwa kulipa mara kumi ya gharama za nyara alizokutwa nazo lakini katika suala hilo mahakama inakaa kimya kwa kuwa haiwezi kutoa adhabu isiyotekelezeka.
Aidha ameongeza kuwa iwapo upande wa mashtaka ukidhibitisha kuwa mshtakiwa anamali ambazo zinaweza kutaifishwa walete maombi mahakamani.
Alisema Maliasili ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo ndio Eden tuliyonayo watanzania ambayo tunapaswa kuiheshimu n kuifurahia wote siyo mtu mmoja mmoja, haiwezekani kuachiwa MTU afanye anachotaka kwani maliasili hizi hutuletea fedha za kigeni.
Ilidaiwa kuwa Juni 28, 2015 huko Mabibo external, washtakiwa walikutwa na vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamani y milioni 600 ambavyo ni sawa na tembo wawili.
No comments:
Post a Comment