Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya kujifungulia,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya Shinyanga vijijini na Kishapu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.
Mbunge
huyo amekabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha afya Tinde,zahanati
ya Solwa,zahanati ya Nyashimbi,kituo cha afya Samuye katika halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga vijijini na kwa upande wa Kishapu ni Kituo cha
afya Nhobola,Mwang’haranga,Dulusi na Songwa.
Vifaa
hivyo vinatokana na jitihada zilizofanywa na mbunge huyo Azza Hilal
Hamad kufika katika ubalozi wa China nchini Tanzania kuomba asaidiwe
vifaa tiba hivyo ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto mkoani
Shinyanga.
Akizungumza
leo Jumamosi May 13,2017 wakati wa kukabidhi vitanda vitatu vya kisasa
vya kujifungulia,vitanda 9 vya wagonjwa na viti vitatu (wheel chairs)
vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 katika kituo cha afya Tinde
kilichopo Shinyanga vijijini,mheshimiwa Hamad alisema vitasaidia
kupunguza adha ya upungufu wa vitanda katika kituo hicho kilichojengwa
mwaka 1920.
“Kituo
cha afya Tinde kinahudumia tarafa yote ya Itwangi na kata za
jirani,kilikuwa na upungufu wa vitanda 28,leo nimeleta vitanda hivi
kusaidia wananchi wapate huduma bora,naomba wananchi muwe mstari wa
mbele kuunga mkono shughuli za maendeleo,ni aibu kuona kituo hiki
kilichojengwa kabla ya uhuru kikiwa hakina majengo ya kutosha ikiwemo
nyumba za watumishi na wodi kwa ajili ya wagonjwa”,alieleza Hamad.
Mwandishi
wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati mheshimiwa Azza Hilal Hamad
akikabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Tinde,ametusogezea picha 3 za matukio yaliyojiri…Tazama hapa chini
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipokelewa kwa shangwe katika kituo
cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini alipofika kukabidhi vitanda
vya kisasa na viti vya wagonjwa vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7
Wacheza
ngoma ya Kiswezi “Waswezi” wakimpokea mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM)
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwahutubia wakazi wa kata ya Tinde
wakati akikabidhi vifaa tiba hivyo
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Wananchi wakimsikiliza mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akiwasisitiza wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo
kujitokeza kuchangia ujenzi wa majengo katika kituo cha afya Tinde
ambacho kilijengwa mwaka 1920 lakini mpaka sasa hakina majengo ya
kutosha
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwataka watoa huduma katika kituo
cha afya Tinde na wananchi kutunza vifaa tiba alivyokabidhi katika kituo
hicho
Viti vya wagonjwa,vitanda vya
kujifungulia kwa akina mama na vitanda vya kulalia wagonjwa
vilivyotolewa na mbunge Azza Hilal kwa ufadhili wa ubalozi wa China
nchini Tanzania
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa Tinde
Vitanda vikiwa eneo la tukio
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha afya Tinde,Dkt. Dama s Mnyaga
Nyansira,shuka kwa ajili ya vitanda vya kulalia wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
akikabidhi vitanda vya kujifungulia akina mama,vitanda vya wagonjwa na
viti vya wagonjwa
Mtoto akiwa amekaa katika kiti cha
wagonjwa wakati mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza
Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akikabidhi vifaa
tiba katika kituo cha Tinde
Wananchi wa Tinde wakimpa zawadi ya
Kondoo,mbunge Azza Hilal Hamad baada ya kufurahishwa na zawadi ya
vitanda na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Tinde
Furaha ikaendelea kuonekana-Mkazi wa Tinde akiwa amembeba mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Wakazi wa Tinde wakifurahia na mbunge wao
Diwani wa kata ya Tinde Japhary Kanolo akizungumza katika kituo cha fya Tinde
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Katibu
wa Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Abdallah Kirobi akimshukuru
mheshimiwa Mbunge Azza Hilal Hamad kuwakumbuka akina mama kwa kuwaletea
vitanda vya kisasa vya kujifungulia
Katibu
wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Secilia Ismail akizungumza katika
kituo cha afya Tinde ambapo alisema Mbunge Azza Hilal Hamad ni mbunge
anayetakiwa kuigwa katika jamii kwani anajua thamani ya maendeleo na
anajali wananchi
Watoa huduma katika kituo cha afya Tinde na wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salum akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Mganga
mkuu wa wilaya ya Shinyanga vijijini Dkt. Amos Mwenda akimshukuru
mbunge Azza Hilal Hamad kwa kuwakumbuka akina mama wa wilaya ya
Shinyanga kwa kuwaletea msaada wa vifaa tiba kwani zahanati na vituo vya
afya vinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo msaada huo utasaidia
kupunguza adha wanazopata wa akina mama na wagonjwa
Wakazi wa Tinde wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Watumishi katika kituo cha afya Tinde wakisoma taarifa ya kituo hicho,Kulia ni Peter Zabron,mwingine ni Mary Joseph
Burudani ikaendelea- Waswezi wakiimba na kucheza
Mtaalam wa Mashairi Anthony Meja akisoma shairi kwa ajili ya Mheshimiwa Azza Hilal
Msanii
wa nyimbo za asili Mama Ushauri akiimba wimbo wa kumpongeza mheshimiwa
Azza Hilal Hamad kwa kutoa msaada wa vitanda kwa ajili ya vituo vya afya
na zahanati mkoa wa Shinyanga
Mbunge Azza Hilal Hamad akicheza na Mama Ushauri
Burudani inaendelea
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikumbatiana na Msanii Mama Ushauri
Wanenguaji wa msanii Mam Ushauri wakicheza kwa madoido
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakionesha mbwembwe zao wakati wakitoa elimu ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa njia ya vituko
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakiendelea kuonesha mbwembwe zao.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment