Wednesday, May 3, 2017

MAONYESHO YA SITA YA MADINI YA VITO YAANZA RASMI LEO JIJIJI ARUSHA


Na Woinde shizza,Arusha

Wananchi wengi wanaoishi karibu na migodi inayochimba madini ya aina mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kupitia madini hayo kutokana na viongozi wao wa maeneo husika kutokuwa na mahusiano mazuri na wamiliki wa migodi hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonyesho ya vito na madini yaliofunguliwa leo jijini hapa

Alisema kuwa japo kuwa madini mengi yenye thamani yanachimbwa hapa nchini, lakini ukifuatilia maisha ya wananchi wa maeneo ambayo madini hayo yanatoka hayafanani kabisa,kwani asilimia kubwa ya wananchi hao ni  maskini sana na wengine hawajiwezi

“Asilimia kubwa ya wananchi ambao madini hayo yanachimbwa ukifuatilia maisha yao ni duni,hawana maendeleo yoyote ,kwa ufupi hawanufaiki na madini ambayo yanatoka katika maeneo yao,hivyo ni wajibu wa Serikali kuangalia upya sera ya madini, Mfano mwananchi wa Mererani madini yanachimbwa kwao, lakini ukiangalia maisha anaoyoishi huwezi sema anakaa sehemu inayotoka Tanzanit”alisema Milya

Naye kaimu naibu katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini James Mdoe alisema kuwa sera ipo na sheria ipo ya kuhakikisha wananchi ambao wanazunguka maeneo ya migodi wanasaidiwa na migodi hiyo, lakini ukifuatilia kwa kiasi kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa mtaa au kijiji hawana ushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao ,hivyo ni wajibu wa wananchi pamoja na viongozi kushirikiana kwa pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia.

Akizungumzia maonyesho haya ya madini ya vito (Arusha Gem Fair )alisema kuwa haya ni maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku tatu,lengo ikiwa ni kutimiza dira iliopo katika sera ya madini ya mwaka 2009 inayosisitiza kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini .

Alisema kuwa sekta ndogo ya vito inachangia katika uchumi wa maendeleo ya jamii hivyo maonyesho haya ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa hapa nchini kuweza kupata fursa ya kujitangaza zaidi 

“Wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wanahudhuria katika maonyesho haya,wengine wanakuja kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe, kwa hiyo hii ni fursa ya pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa zaidi waangalie ni namna gani watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema Jemsi
baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho


Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini Arusha(habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
Meya wa jiji la Arusha naye aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini 

No comments: