Monday, May 22, 2017

MAMIA YA WAKAZI WA KIGOMA WAJITOKEZA KUPATA MATIBABU YA MADAKTARI BINGWA.

 
 Anna Makinda ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya(NHIF)akiongea na wagonjwa waliofika leo hospital ya Mkoa wa kigoma kwaajili ya kupata matibabu toka kwa madaktari bingwa.
 Anna Makinda akikata upete katika hospita ya Mkoa wa Kigoma kuzindua zoezi la utoaji wa huduma kwa madaktari bingwa kwa hospita za pembezoni
 Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya(NHIF)Anna Makinda akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika katika hospita ya Mkoa wa Kigoma(maweni)kwaajili ya kupata huduma za madaktari bingwa.
 
 
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.


MAMIA ya wananchi wa mkoa Kigoma wamejitokeza katika kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika mpango unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF).matibabu hayo yanayotolewa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni yanahusisha magonjwa ya kina mama ,magonjwa ya moyo,magonjwa ya watoto ambayo madaktari bingwa wake watafanya kazi hiyo moja kwa moja huku magonjwa mengine ambayo hayana madaktari bingwa utatolewa ushauri wa hatua za kuchukua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo,Anne Makinda alisema kuwa hakuna mtanzania atakayekufa kwa sababu ya kukosa pesa za matibabu kutokana na serikali kuweka mfumo mzuri unaohakikisha wananchi wote wanapata matibabu kwa gharama nafuu.

Makinda alisema kuwa kwa sasa wananchi wote wataweza kujiunga na huduma za matibabu za mfuko huo kupitia makundi mbalimbali yalipo kwenye jamii na mitaa na wananchi watapata huduma za matibabu nchi nzima bila kubagua hospitali.

Alisema kuwa pamoja na hilo mfuko huo unatambua kuwepo kwa changamoto za uhaba wa madawa,vitendea kazi,uchache wa majengo na vifaa vingine vya kutolea tiba na kwamba mfuko huo umzingatia changamoto hiyo na kwa sasa mfuko unatoa mikopo kwa vituo vya afya,zahanati na hospitali ili kuwezesha huduma bora kupatikana wakati wote.

Akizungumzia utoaji huduma kwa wagonjwa alisema kuwa mfuko unapokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na lugha mbaya na za kuudhi zinazotolewa na watoa huduma na kwamba ikithibitika kwamba yupo mtoa huduma ametoa lugha mbaya kwa wagonjwa watachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.

Awali wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bernad Konga alisema kuwa mfuko unatambua changamoto iliyopo ya uhaba wa madaktari bingwa uliopo nchini na ndiyo maana mfuko umeanzisha mpango wa huduma za madaktari bingwa wanaotembea ili kuweza kuwafikia wananchi.

Pamoja na kutoa huduma kwa wananchi Konga alisema kuwa mpango huo pia unalenga kutoa mafunzo kwa watoa huduma waliopo kwenye vituo ambavyo mpango huo unatekelezwa ili waweze kuendeleza huduma husuka baada ya madaktari bingwa hao kuondoka.

Alisema kuwa tangu kuanza kwa mpango huo jumla ya wananchi 13,000 wamfikiwa na kati yao zaidi ya 600 wamepatiwa huduma za upasuaji wa magonjwa mbalimbali na hivyo kufanikisha mpango wa kuwafikia wananchi kwa karibu.

Akizungumza kabla ya kuzindua mpango huo Mkuu wa mkoa Kigoma,Emanuel Maganga alisema kuwa kumekuwa na uhitaji wa madaktari bingwa mkoani humo ikizingatiwa kuwa kwa sasa mkoa unao madaktari bingwa wawili tu jambo ambalo linafanya wananchi kutumia muda na gharama kubwa kutafuta huduma hizo nje ya mkoa.

Alisema kuwa mpango huo ni wa maana sana kwani utawasaidia wananchi wa mkoa huo kupunguza makali ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakati huu na kwamba serikali ya mkoa itatoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unakuwa wa mafanikio.

No comments: