Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa 5 wa Chama cha Makatibu
Mahususi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa
mikutano wa Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Sehemu
ya wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi
Tanzania (TAPSEA) ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan(kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi
na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki leo kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu
wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza Makatibu Mahsusi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
na waache tabia ya kutoa siri za ofisi zao kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ametoa kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu
Mahsusi Tanzania katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mji Dodoma.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia
pekee ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi
nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya
kazi.
Makamu
wa Rais pia amewahimiza makatibu mahsusi kufanya tathmini ya utendaji
wao wa kazi na wawe tayari katika kujifunza mbinu mpya za utendaji
zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.
“Sote
tunafahamu kuwa dunia imekuwa ni kijiji kutokana na utandawazi
unaoletwa na mifumo ya teknolojia hivyo kutokana na mabadiliko haya
hamna budi nanyi kubadilika na kwenda na wakati ili msiangaliwe kwa
mtazamo hasi wa kuwa wapiga cha tu”
Kuhusu
uanzishwaji wa Shahada ya Uhazili, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amewahakikishia makatibu mahsusi kuwa Serikali imekubali
kuanzisha shahada hiyo ambapo masomo yake yataanza mwezi wa Tisa mwaka
huu kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika mikoa ya Dar es
Salaam na Tabora.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza makatibu mahsusi
kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu kwa kuzingatia
kuwa elimu haina mwisho.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema Serikali inafanyia kazi
baadhi ya kero zinazowakabili makatibu mahsusi ikiwemo kuboresha maslahi
ya kada ya uhazili nchini.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakikisha kada hiyo pamoja na watumishi wengine
wanapata maslahi bora ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika
kuongeza ufanisi kazi.
No comments:
Post a Comment