KAMPUNI ya vifaa vya Umeme ya Life is Good (LG) imezindua viyoyozi ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa gharama
za kuweza kumuda kwa kila mtanzania.
Akizungumza na katika hafla ya uzinduzi wa viyoyozi hivyo , Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa
Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma amesema vifaa vya LG vina
ubora katika matumizi ya nishati ya umeme.
Amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni
muhimu kutumia vifaa vya umeme ambavyo
ni rafiki wa mazingira bila kufanya hivyo itakuwa tunaharibu mazingira kwa vizazi
vijavyo.
Amesema kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi hakuna mtu anayeweza kukwepa katika kutumia vifaa ambavyo vinakuwa
ni rafiki wa mazingira.
Nae Mkurugenzi Mtendaji LG
Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung,
amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona kuna mahitaji ya viyoyozi
ambavyo vitakuwa ni rafiki wa mazingira na kutaka watu watumie bidhaa hiyo.
Amesema viyoyozi hivyo vinatumia
nishati ndogo hali ambayo inafanya kila mtu kuweza kumudu matumizi ya viyoyozi pamoja
na kulinda mazingira.
Aidha amesema kuwa watu wanatakiwa
kutumia vifaa ambavyo vinakuwa rafiki wa mazingira ambapo LG wameweza kuzalisha
bidhaa kutokana na mahitaji ya sasa yaliyopo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa
Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi wa viyoyozi iliyofanyika leo
katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics
Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa
viyoyozi vya LG iliyofanyika leo katika
Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG
Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira .
Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania , Ramachandran Veeraman
Watumbuizaji wa bendi ya Borabora wakiwa wanatoa burudani jukwaani
Bendi ya muziki ya Borabora ikitoa burudani kwa watu waliofika katika mkutano huo
sehemu ya wafanyakazi wa LG wakiwa katika picha ya pamoja
1 comment:
Hizi bidhaa za LG kiukweli zina ubora wa hali ya juu sana, haswa TV zake, simu zake, friji zake, AC zake na microwave zake, kwa sababu kwenye bidhaa hizi, Mchina hapa bado hajatia mkono!. Unaweza kununua Sony ukijua ni Sony au Samsung ukijua ni Samsung, kumbe ni mchina fulani!, lakini ukinunua LG, umenunua LG kweli!.
Asante
Pasco
Post a Comment