Monday, May 29, 2017

JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI



FO1
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Chole katika kituo cha Afya Chole. 
FO2
Gari la wagonjwa lilokabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Chole
FO3
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kituo cha Afya Chole pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mara baada ya Kukabidhi gari la wagonjwa.
FO4
Jengo la Zahanati ya Visiga
………………………………………………..

Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi wote pamoja na wananchi wa wilaya ya kisarawe katika ujenzi wa zahanati Mpya 11 pamoja na wodi 2 za wazazi.Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe alitoa pongezi hizo alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni Kisarawe.

Ujenzi huo unafanyika kupitia fedha za mfuko wa jimbo ambazo zimetumika kununua saruji na mabati na pia  fedha kutoka Halmashauri ya wilaya ya kisarawe na michango ya wananchi.

Akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati ya visiga, Jafo alipongeza wananchi wa visiga kwa kuunga mkono juhudi ya serikali ya awamu ya tano katika kujileta maendeleo.Aliwaomba viongozi wote waendelee na moyo huo huo wa mshikamano ili kufanikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2015.

Katika hatua nyingine, Wananchi wa Tarafa ya Chole wilayani Kisarawe wameishukuru serikali ya awamu ya tano baada ya Mbunge wa jimbo la Kisarawe na Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tamisemi kukabidhi gari la wagonjwa aina ya Toyota Landcruiser kwa Kituo cha Afya chole.

Wananchi hao waliishukuru serikali na Mbunge wao kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo ikiwemo kushughulikia matatizo ya afya.

Tarafa hiyo ina kata tatu ambapo wananchi wake walikuwa hawana gari ya wagonjwa na hivyo kukabiliwa na changamoto hasa akina mama wanapotaka kwenda kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambayo ipo umbali wa zaidi ya kilomita 100.

Wananchi hao walisema serikali imedhihirisha wazi kuwajali wananchi hao walioteseka kwa muda mrefu huku wakifurahia mipango ya serikali ya kukarabati Kituo cha Afya  Chole kwa kujenga Jengo Maalum la Upasuaji pamoja na kuliwekea vifaa vyote, na ujenzi wa wodi za wagonjwa mradi unaotarajiwa kugharimu wastani wa shilingi milioni 700.

Mmoja wa wananchi hao, Mama Makwega alimshukuru sana mbunge Jafo na kumwagia sifa Rais Magufuli kwa kuwajali wananchi wote nchini Tanzania.

No comments: