Tuesday, May 16, 2017

EFM REDIO YAMTUNZA MAMA

Katika kuazimisha siku ya mama duniani Efm redio kupitia kipindi chake cha uhondo wametoa zawadi kwa  wakina mama wa wasikilizaji wao katika tafrija fupi iliopewa jina la “Begi la mama”. Tafrija hiyo ilifanyika katika ofisi za efm redio siku ya Leo kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 Alasiri.  Begi la mama lilitolewa kwa wakina mama 15 ambao stori zao ziliandikwa na watoto wao na kuonekana kugusa mioyo ya wasikilizaji wengi kwa yale magumu waliopitia.
  Mtayarishaji wa kipindi cha uhondo Asha manga akipeleka begi la mama likiwa limejaa zawadi kem kem
 Timu nzima ya kipindi cha Uhondo ikiongozwa na Dina Marios wakimtunza mama nguo kutoka katika begi.
 Muda wa chakula ukafika.
 Mtangazaji wa kipindi cha uhondo akimuhoji mshindi ambae alikuja na mama yake kwaajili ya kuzawadiwa begi hilo.
 Mama akiwa kashikilia zawadi alizotunzwa na Efm redio.
 Timu nzima ya kipindi cha uhondo ikiongozwa na Dina Marios mstari wa pili (wakwanza kushoto) akifatiwa na Sofia Amani, Leah Chambo, Rdj Con wengine ni Bi, Hindu, Swebe Santana, Asha manga, na wengineo.


No comments: