Wananafunzi
wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla,
wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada
na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama
Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya
Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba
iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi
kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza
wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi
Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz).
Awali
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa
Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya
maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana
mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru
akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu
kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau
wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa
akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline
Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na
lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi
za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi
Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya
kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada
wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi
Hananasifu.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja
na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya
Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi
akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya
kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma
moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi
Makumbusho waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi na Afisa
Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya
Kinondoni kwa pamoja wakizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya
maktaba hiyo. Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim (wa pili kulia) Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Makumbusho wakisoma vitabu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Dr. Ntuyabaliwe Foundation
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama
Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule
wakikagua vitabu katika maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo (katikati) akionyesha
waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) muonekano wa
awali kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation.
Kushoto ni Mama Mengi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Shule, Haji
Shabani Kibwana
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi
akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya
kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika
shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini
kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi.
Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa
Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi
akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama
Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho
kabla ya uzinduzi huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la
uzinduzi wa maktaba hiyo
No comments:
Post a Comment