Tuesday, May 2, 2017

102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’


Mkurugenzi wa 102.5 Lake FM, Doreen Estazia Noni akiiunua mfuko wa takataka na mtangazaji wa a kituo hicho Tatu Rajab wakati wa zoezi la kusafisha jiji la Mwanza lijulikanalo kwa jina la Ng'arisha Nzengo, Uchafu Nuksi. Zoezi hilo litakuwa linafanyika mara kwa mara.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. 
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Katibu wa wenyeviti wa mitaa jiji la Mwanza, Hamza Shido akishiriki katika kampeni hiyo ya 'Ng'arisha Nzengo' iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102​.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishangilia mara baada ya kuhitimisha kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza ijulikanayo kwa jina la 'Ng'arisha Nzengo'.
 
 Kituo cha Redio cha 102.5 Lake FM kimezindua kampeni ya kufanya usafi kwa jijini la Mwanza ijulikanayo kwa jina la  Ng’arisha Nzengo, Uchafu Nuksi yenye lengo la kuufanya mji huo kuwa msafi zaidi.

Mkurugenzi wa kituo hicho Doreen Estazia Noni amesema kuwa wameamua kuanzisha kampeni hiyo ya usafi ili kuupendezesha zaidi mji huo ambao ni minongoni mwa miji mikubwa hapa nchini.Doreen amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Lake Fm nikuhakikisha inatoa mianya ya kuiwezesha jamii kufikia kusudi la maendeleo binafsi na jamii nzima kwa ujumla.

“Neno ni la kabila ya Wasukuma lenye maana ya nyumbani, tumeamua kutumia neon hili ili kufikisha ujumbe haraka kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kampeni hii ni  endelevu kituo chetu cha redio kitaendelea kuhamasisha mpaka kufikia lengo letu,” 

“Kituo chetu cha redio kimeamua kupanua wigo wake kwa kujihusisha katika masuala mbalimabli ya kijamii na kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mtazamo chanya na si kuhabarisha na kuburudisha tu,   naomba ushirikiano mkubwa kwa wadau,  serikali na watu  binafsi katika kufanikisha kampeni hii,” alisema Doreen.

Mbali ya 102.5 Lake FM, kampeni hiyo pia imewashirikisha wadau wengine kama Baamedas tv, Genic Studios , viongozi wa Jumuiya ya biashara ndogondogo, minada na masoko , mwenyekiti Justin Sagala, mwenyekiti wa Afya Minadani, Gosbert Lucas, katibu wa afya, Mariam Magembe, kiongozi wa wa madereva  wa daladala  Dede Petro, serikali na Asasi binafsi.

Mkuu wa maudhui na vipindi  wa redio hiyo,  Yusuph Magupa ambaye pia ni mwenyekiti wa kampeni hiyo amesema kuwa  afya ni ghali na wakazi wa Mwanza wanapaswa kuishi katika mazingira salama ili kulinda afya yako.

Kupitia uzinduzi wa kampeni hii iliyozinduliwa rasmi siku ya jumatatu ya Mei Mosi, katika kipindi cha asubuhi cha Kokoliko, Magupa amebainisha mpango mkakati wa kampeni hiyo kuwa nikuhakikisha elimu ya usafi kwa afya bora inaeleweka na kuzingatiwa katika jamii.

Katibu wa kampeni hii, Iman Hezroni ambaye ni pia ni mtangazaji  wa redio hiyo amesema kuwa mbali ya wao, kampeni pia imewashirikisha wakazi wa Mwanza kwa asilimia kubwa ili kuzidi kujenga mahusihano mazuri baina ya kituo na wananchi.

Hezron amesema 102.5 Lake Fm itahakikisha inatoa fursa kwa wanajamii kusikika na kueleza matakwa yao ili kutafuta mikakati ya matakwa yao kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa kituo redio hiyo ipo kwa ajili wananchi.

Alisema kuwa  Mkurugenzi wa kampuni ya 102.5 Lake Fm  kwa sasa anafanya mazungumzo na  Jumuiya ya biashara ndogo ndogo, minada na masoko ambapo maazimio yaliyofikiwa ni kuijenga ziara maalum ya kuitembelea minada  yote ndani ya jiji la Mwanza, iliyopewa jina la Gulio la mtaa.


Alifafanua kuwa dhamira ya ziara hiyo nikusogeza elimu ya usafi katika maeneo hayo,uboreshaji wa huduma ya vyoo minadani pamoja na maboresho ya kimiundombinu katika minada kupitia Gulio la mtaa lakini pia litatimiza zana ya kupeleka radio kwa wananzengo, kwa kuhakikisha inawaburudisha na muziki wa kisasa pamoja na ule wa asilia.

No comments: