Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.
Na Ripota wa mafoto Blog, Dar
WITO
umetolewa kwa wananchi wa kipato cha
chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa
jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto,
Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali
wananchi wa aina zote.
Aidha
alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo
la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.
Bima
hiyo imelenga zaidi kuwafikia wananchi wote haswa wale waso na kipato kikubwa na
wa kipato cha kati ili wote wanufaike na huduma za afya.
Mbanga
alitoa wito kwa wananchi wengi kutumia fursa hiyo ili kuweza kuwekeza fedha
ambazo wanazitumia kwa matibabu kwaajili ya mahitaji mengine ya kiuchumi.
“Pamoja
na kwamba kuna sera mbalimbali za afya zinazozungumza juu ya upatikanaji wa
huduma za afya kwa njia rahisi, lakini bado bila bima ya afya wagonjwa wengi
watapoteza maisha kwa sababu kuna
watanzania wengi ambao hali za kipato
chao sio nzuri.
Ni
vyema wananchi wengi wakajiunga na mfuko huu wa bei nafuu ili kile kiasi
kilichokuwa kikitumika kufanya matibabu wakiwekeze kwenye shughuli nyingine za
uchumi,”alisema.
Aidha
alisema asilimia 27 tu, ndio wamejiunga na mfuko hivyo kuna wananchi wengi
ambao hawajajiunga na mfuko huo.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Group na Zurich Insurance Brokers (EA)
Sudi Simba alisema, huduma hiyo ilianzishwa mwezi Aprili mwaka jana, lengo
likiwa ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini na kati, ambapo kwa kila
familia ya watu wanne wataweza kukatiwa bima kwa sh.174,000 tu.
“Watu
hawa ni baba, mama na wategemezi wao ambao ni watoto chini ya miaka 18 .
Bima
hii kama kuna uhitaji wa kuongeza wengine unapaswa kulipia sh. 100,000 kwa
mwaka kwa kila atakaeongezeka,”alisema.
Khadija Kopa na kundi zima la bendi ya TOT wakitoa burudani na kuimba wimbo maalum uliotungwa nao kuhusu Bima hiyo mpya.
Mgeni rasmi akihojiwa na waandishi baada ya uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment