Kampeini
ya Taifa Moja inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa matamasha
ambayo yatafanyika kwenye mikoa mitano hapa nchini ikiwa na lengo ya
kuendelea kutoa burundani pamoja elimu kwa Watanzania juu ya kutuma na
kupokea fedha kutoka kwenye mtandao wowote kwa gharama ile ile.
Taifa
Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector
Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates
Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC)
chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel
Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money,
Tigo Pesa na Ezy Pesa.
Akizungumza
jijini leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi
wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa
matamasha hayo alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba
Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali
hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda
mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.
Milinga
alitajwa mikoa ambayo matamasha hayo yatafanyika ni pamoja na Mbeya
(Mwenge Primary School), Dar es Salaam (Zakhiem Grounds), Arusha
(Kilombero Grounds), Mwanza (Furahisha Grounds na Tabora (Uyui Grounds)
huku msanii Chege akitumbuiza Mwanza, Stamina na Jambo Squad
wakitumbuiza Arusha, Belle 9 Mbeya, Cassim Mganga Tabora huku Mkubwa na
wanae wakifanya yao Jijini Dar es Salaam. Matamasha hayo yatafanyika
Jumapili ya tarehe 16 April mwaka huu.
Kuhusu
kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma ya kutuma na kupokea pesa kwenda
mtandao kwa gharama ile ile Meneja Chapa kutoka kampuni ya Tigo
Tanzania William Mpinga, Moses Alphonce ambaye ni Meneja wa Airtel
Money, Patric Dumulinyi ambaye ni Mobile Money Manager walitoa wito kwa
wananchi kwenye mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwani matamasha haya ni
ya wazi na hakuna kiingilio.
‘Natoa
wito kwa Watanzania kujitokeza na kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya
kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote kwa gharama ile ile,
alisema,’ alisema Mpinga.
Mpinga
alisema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kupunguza gharama za kutuma
fedha kwenda mitandao mingine na upotevu wa fedha uliokuwa ukijitokeza
hapo awali.
Alisema
kampeni ya Taifa Moja itaongeza uelewa wa watumiaji wa simu za mikononi
nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja
kwenda mwingine kwa gharama ile ile.
“Watumiaji
wa huduma za simu-pesa watatumiana pesa kutoka mtandao mmoja kwenda
mwingine na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti za simu –pesa ya mteja
aliyetumiwa, hakutakuwa na sababu ya kuhofia pesa hiyo uliyotumiwa
kwenda kuitoa haraka ukihofia kumrudia aliyekutumia kama ilivyokuwa hapo
awali," aliongeza Moses Alphonce kutoka Airtel Money.
Kwa
upande wake, Rukia Mtingwa ambaye ni Meneja Chapa na Mawasiliano
alisema njia hii ya sasa ni tofauti na utaratibu wa zamani ambao mteja
akimtumia mwenzake ambaye yupo mtandao mwingine hutumiwa ujumbe wa
meneno (sms) kwa aliyetumiwa kwenda kuchukua pesa hiyo kwa wakala.
“Kuanzia
sasa tutaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa mitandao yetu juu ya
utumaji pesa kutoka kwenye mtandao mmoja kwenda mwingine anavyoweza
kukatwa kiasi cha fedha kile kile kama ambacho angelikatwa kutoka
mtandao kama wake.”Aliongeza Mtingwa.
No comments:
Post a Comment