Wednesday, April 19, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema kukua kwa sekta ya Utalii visiwani humo isiwe sababu ya kupoteza Historia ya Zanzibar; https://youtu.be/5NAnCIxiU2E

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imeitaka mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia riba zake upya ili kuwawezesha wananchi wengi kujikwamua kiuchumi; https://youtu.be/53zYSlxorBk

SIMU.TV: Shirika la maji safi na maji taka jijini Dar Es salaam DAWASCO limetakiwa kuhakikisha linamfikishia maji kila mwananchi anayeishi katika jiji hilo; https://youtu.be/GT-F4qSKQk0

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo katika soko la Kariakoo wameitaka Dawasa kuhakikisha wanaweka mazingira ya mitaro safi na salama; https://youtu.be/Rc3WoMw4rVQ

SIMU.TV: Shule ya msingi ya watoto wasioona ya Malangali iliyoko kwenye manispaa ya Sumbawanga inawaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia; https://youtu.be/NprvGWs66wU

SIMU.TV: Wafanyabiashara wa vyakula maarufu kama Mama Lishe mkoani Mtwara wamelalamikia kitendo cha kutozwa fedha za Takataka ambazo hazizolewi; https://youtu.be/MtGCjbGAnBg

SIMU.TV: Serikali imeombwa kuingilia kupanda holela kwa bei ya mahindi kunako sababishwa na baadhi ya wafanyabiashara kuficha mahindi; https://youtu.be/sghIjK_Pwm8

SIMU.TV: Wafanyabiashara na abiria wanaotumia kituo cha Mwenge jijini Dar Es salaam wameiomba Sumatra kuweka kituo rasmi katika eneo hilo la Mwenge; https://youtu.be/bTynQf18190

SIMU.TV: Kamati ya sheria, katiba na hadhi za wachezaji ilikua na kikao leo jijini Dar Es salaam kuchunguza kiundani maamuzi ya kamati ya masaa 72 kuipatia Simba pointi tatu; https://youtu.be/1Sv9apyxWJ4

SIMU.TV: Timu ya Simba ya Dar Es salaam imeibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya timu ya Rhino Rangers ya mkoani Tabora; https://youtu.be/AuVXPSRc540

SIMU.TV: Mashabiki wa klabu ya Yanga mkoani Iringa wana imani kuwa klabu yao itapigana kiume na kutetea Ubingwa wake kama kawaida; https://youtu.be/RKF5wHBWhO4

SIMU.TV: Fahamu hapa habari motomoto tulizobahatika kukukusanyia kwa siku ya leo kunako anga za michezo Kimataifa; https://youtu.be/oJ_xAAXp0Mg

SIMU.TV: Waziri wa nchini Tamisemi George Simbachawene amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa wizara yake mwaka 2017/2018; https://youtu.be/8V5CCE09yx4

SIMU.TV: Uhaba wa wataalamu katika sekta ya Afya nchini Tanzania imetajwa kuwa kikwazo kimoja wapo katika safari ya maendeleo kwa nchi; https://youtu.be/CNYoI7INZOU

SIMU.TV: Jeshi la polisi visiwani Zanzibar limefunga baadhi ya vituo vidogo vya polisi ili kuvipa nguvu vituo vikubwa vya polisi visiwani humo; https://youtu.be/Nm7u7lUPC9Q

SIMU.TV: Wazee na Vijana wilayani Kakonko mkoani Kigoma wameungana na kuamua kuanzisha mradi wa ufugaji Samaki ili kujikwamua kiuchumi; https://youtu.be/M-Qjjx9k82k

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuweka wazi majukumu yake ili kuongeza uaminifu kwa wananchi; https://youtu.be/Tlhpj4-ZacU

SIMU.TV: Watu watatu kati ya kumi na mbili wamejeruhiwa katika ajali mbaya ya Bus iliyohusisha Bus la Abood lililokuwa likisafiri kutoka Arusha kwenda Morogoro; https://youtu.be/bpghui7MiS0

SIMU.TV: Wadau wa sekta binafsi nchini TPSF wameiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza vikwazo vya biashara nchini; https://youtu.be/6MVaszHoF7I

SIMU.TV: Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi NEEC limewataka watanzania kuchangamkia kununua Hisa za Vodacom; https://youtu.be/3hbYs9jiocg

SIMU.TV: Fahamu hapa mauzo ya Hisa katika soko la Hisa la Dar Es salaam DSE ambapo tunaambiwa mauzo yameshuka kidogo; https://youtu.be/WbI1z2k0GCA

SIMU.TV: Kamati ya haki sheria na hadhi za wachezaji ya TFF bado inaendelea na kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Kagera Sugar ikipinga kupokwa alama tatu. https://youtu.be/UsDNBXvHW5c

SIMU.TV: Kundi la pili la wachezaji wa klabu ya Yanga lililokuwa limechelewa ndege limewasili nchini leo huku wakiwakimbia waandishi wa habari. https://youtu.be/qXop7I02a8s

SIMU.TV: Usiku huu katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Bayern Munich wanatarajiwa kuwafuata Real Madrid kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali. https://youtu.be/LDWXjry9edI

No comments: