Thursday, April 27, 2017

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA SHINDANO LA MASAA 48 ILI KUITANGAZA ABU DHABI KWA WASAFIRI


Mohammad Al Bulooki, Makamu wa Rais Mtendaji wa Kitengo cha biashara cha Shirika la ndege la Etihad; Mhe. Saif Saeed Ghobash, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Utalii na Utamaduni (TCA) Abu Dhabi, Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege la Etihad wakisheherekea uzinduzi wa ndege shindano la masaa 48 la kuitangaza Abu Dhabi katika Soko la usafiri la Uarabuni.

Msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson akiruka matuta ya jangwa la Abudhabi wakati aliposhiriki shindano lililozinduliwa na Etihad la masaa 48 ili kuitangaza Abudhabi kwa wasafiri wake.



Wakazi wa Nchi ya Falme za Kiarabu na wasafiri wa kimataifa watajionea maeneo mbalimbali ya vivutio vinavyopatikana Abu Dhabi kwa siku mbili tu.

v Shirika la Ndege limezindua shindano hilo kwenye Instagram na zawadi zaidi ya 500 zitashindaniwa.

Shirika la Ndege la Etihad limeamua kuwazawadia mamilioni ya wageni wanaosafiri kupitia makao makuu pamoja na wakazi wa nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuleta shindano linalofanyika angalau mara moja kwa mwaka na kuwahusisha watu wote kwa siku mbili.

Kampeni hiyo ya 48 Hour Challenge ni sehemu ya shughuli za Etihad katika kupanua wigo wa kuitangaza Abu Dhabi kama sehemu nzuri ya mapumziko kwa wasafiri na watu wanaopenda kuishi katika nchi ya Falme za Kiarabu hasa wanaopenda kutembelea wakati wa likizo fupi. Wakiwa kwenye jiji hilo watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yameandaliwa kupitia programu hiyo.

Kampeni hiyo ya Shirika la Ndege la Etihad itazinduliwa na msanii maarufu kutoka Uingereza anayetambulika kwa jina la Rick Wilson ambaye atatangaza jinsi watu wanavyoweza kunufaika na ofa hiyo ya saa 48 wakiwa Abu Dhabi.

Baadhi ya video zake zitaonyesha ofa katika maeneo ya vivutio vya Abu Dhabi. Pia, video za kampeni hiyo zitaonekana kupitia mtandao ambapo wateja watashare na wenzao katika mitandao ya kijamii. Pia wataweza kuona kupitia chaneli za kwenye ndege wanaposafiri.

Wilson alisema, “Kwangu mimi nilijua hii inaamanisha kukaa uwanja wa ndege, au kusafiri bure lakini sivyo kampeni hiyo inavyomaanisha.”

“Mtu atapata fursa ya kusafiri katika ukanda wa jangwa ikiwa ni pamoja na kutembela maeneo ya kuvutia ya kiutamaduni. Abu Dhabi imenifunza kuwa kutembelea maeneo mbalimbali nikiwa safarini ni sehemu mojawapo ya kuburudika. Hii inaweza kuwa ni miongoni mwa njia nzuri za kupumzika na kujiweka katika hali ya kujisikia vyema. Vilevile nimepata muda wa kujionea mambo mengi kwenye nchi hii. Niwapo safarini sitarudia tena kukaa tu uwanjani na kusubiri ndege tu.”

“Abu Dhabi ni sehemu nzuri, yenye joto kiasi na watu wake wenye ukaribu wa hali ya juu. Mji huu una kila kitu kinachohusiana na mapumziko. Kuna sehemu tulivu na maeneo mazuri ya kutembelea. Ni mji unaovutia na kupendeza ambao una vitu vya kipekee unavyoweza kujionea kwa muda mfupi na kwa wakati.”

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Kuzinduliwa kwa programu hii ya Shirika la Ndege la Etihad kutawawezesha watu kutembelea maeneo mbalimbali wakati wakisubiri kusafiri.
Pia itahamasisha watu kujua zaidi kuhusu jiji hili tunaloishi na kufahamu mambo mengi yanayohusu Abu Dhabi pamoja na kuona fursa zilizopo hususan kwa wageni katika masuala ya utamaduni na maeneo ya kupumzika katika fukwe.”

Alisema, “Ni heshima kwa shirika letu la kitaifa la Falme za Nchi ya Kiarabu ambalo makao makuu yake yapo hapa Abu Dhabi, kutokana na kuwapo kwa miundombinu mizuri, ukarimu kwa watu wake na mazingira mazuri ya kuvutia. Hii ni sehemu nzuri ya kutembelea kwa wote wanaosafiri kupitia Abu Dhabi na pia tumewapa fursa hata wale wanaoishi hapa.”
Shirika hilo limetumia fursa ya kujitangaza kutokakana na kuwepo uzinduzi wa Soko la Usafirishaji Uarabuni. Etihad imebuni mashindano hayo maalumu kwa lengo la kujitangaza.

Kwa mwaka huu mzima wa 2017, Shirika la Ndege la Etihad litatoa jumla ya zawadi 500 na wale ambao watashiriki kampeni ya 48 Hour Challenge watatuma hashtag ya #EtihadChallenge kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Shirika la ndege la Etihad limechagua hoteli mbili Abu Dhabi pamoja na maeneo ya shughuli mbalimbali. Wateja watajishindia kulala usiku mara mbili kutoka kwenye hoteli 60 Abu Dhabi na wengine watajishindia kulala usiku mmoja bure.
Wateja wa daraja la kwanza watapata nafsi kulala bure wakati wateja wa daraja la juu watapata nafasi ya kulala siku mbuli bure.

Wateja wanaotumia ndege ya Airbus A380s watazawadiwa kulala mara mbili usiku katika hoteli ya kisasa ya Emirates Palace.

Abu Dhabi ambayo ndiyo kitovu cha maeneo mazuri ya kupumzika na eneo lenye vivutio vingi vya kibiashara ulimwenguni, kuna eneo kubwa lenye mchanga wa ufukweni, maeneo ya utalii kama vile Yas Waterworld na Ferrari World ikiwa na pamoja na jangwa lenye historia ya kipekee. Pia taasisi ya utamaduni kama vile Manarat Al Saadiyat na hivi karibuni makumbusho ya Louvre yatafunguliwa
Kuna maeneo ya kihostoria, migawaha ya kimataifa, maeneo ya michezo ya gofu, mbio za magari maarufu Fomula 1 Etihad Airways Abu Dhabo Grand Prix na mashindano mengine ya magari ya Yas Marina Circuit.


Abu Dhabi pia inatoa fursa kwa wageni kufanya manunuzi katika maduka makubwa na maarufu. Pia, utapata nafasi ya kuchagua bidhaa kwenye maduka makubwa kama vile Yas Mall, Abu Dhabi MALL, Marina Mall na The Galleria ambayo ni miongoni mwa eneo kubwa ulimwenguni kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa.

Rick Wilson amefanikiwa kumaliza kufanya shughuli zifuatazo kwenye kampeni hii ya Abu Dhabi 48 hours Challenge;-
·        Ametembelea maeneo muhimu ya slingshot
·        Ameshiriki mashindano ya magari
·        Amejionea mashindano ya Formula 1 track
·        Amejionea maporomoko ya maji ya Yas Waterworld
·        Amenunua bidhaa kwenye maduka makubwa
·        Amefurahia kupata kifungua kinywa katika jengo la Etihad Towers
·        Amejionea mchanga wa jangwani
·        Amekula vyakula vya kiasili
·        Amepanda ngamia
·        Amejifunza namna ya kucheza
·        Ametembelea jangwa
·        Amelala kwenye hoteli ya nyota tano
·        Amefika kwenye ufukwe wa Saadiyat Golf Club
·        Ameendesha gari kwenye mashindano ya Formula Rossa, Ferrari World Abu Dhabi
·        Amekula kwenye migahawa ya kiutamaduni
·        Ametembelea Msikiti wa Sheikh Zayed Grand
·        Ametembelea Iris Yas Island
·        Amefika Yas Viceroy

Video ya Ricky Wilson’s 48 Hour Challenge unaweza kuitazama: https://www.youtube.com/watch?v=lhZgRWOQQrw

Unaweza kupata picha za matukio hapa https://we.tl/xXrIF1vBf4 


Kwa maelezo zaidi kuhusu shindano hilo la Etihad Airways’ stopover tembelea: www.etihad.com/abudhabi

No comments: