Tuesday, April 25, 2017

MRADI WA KUHAMASISHA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA UWAKILISHI WA KISIASA (WRPRE PROJECT) WAZINDULIWA

1
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Woman And Youth Political Participation Enhanced In 2019 Aand 2020 General Election In Tanzania uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ,Serikalini. Vyama vya siasa, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za Kiraia.

Mradi huo utakaotekelezwa na Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA na TYC na WE Effect huku ukifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kiasi cha sh ilingi Bilioni 1.4na utatekelezwa kwa miaka mitatu.

Lengo la Mradi huo ni Kuongeza Ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uwakilishi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019-2020 katika ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa, Mradi huu pia unalenga kuangalia vizuizi vinavyokwamisha wanawake na vijana kushiriki kwenye mchakato wa kugombea uongozi wa kisiasa na kuangalia ni jinsi gani vizuizi hivyo vinaweza kutatuliwa.
2
Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Roeland Van De Geer akitoa ujumbe wake kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi huo, Jumuiya ya Ulaya ndiyo iliyofadhili mradi huo .
3
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
4
Mama Anna Mngwira aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 na mwanachama wa Chama cha wanasheria wanawake akifuatilia kwa makini uzinduzi wa mradi huo
5
Baadhi ya waalikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa mashirika na taasisi za serikali.
6
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
7
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka wakati alipowasili kwenye hoteli ya New Africa kwa ajili ya uzinduzi wa mradi huo.
8
Baadhi ya maofisa kutoka TAWLA wakisimamia uasili na kuwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
9
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
10 11 12
Afisa kutoka Makao Mkuu ya CCM Ofisi Ndogo ya Lumumba Bw. Suleiman Mwenda pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
13
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa katika mara baada ya uzinduzi huo.
14 15

No comments: