Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce akitoa elimu kwa mmoja wa watumiaji wamitandano ya simu kwa namna Makampuni
ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na
kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile
ile.
Makampuni
ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na
kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile
ile.
Kwenye
muungano huo ambao unaitwa Taifa Moja, makampuni matatu makubwa ya
kutoa huduma za simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Airtel Tanzania na
Zantel, wateja wanaweza kutuma pesa na kupokea kutoka kwenye moja ya
mitandao hiyo kwa gharama zile zile.
Hapo
awali, kutuma pesa au kupokea pesa kutoka mtandao tofauti mteja alikuwa
akipokea ujumbe mfupi ambao ilikuwa ni lazima apeleke kwa wakala wa
mtandao ambao amepokea fedha kutoka na ilikuwa izizidi siku saba tofauti
na hapo fedha hiyo ilikuwa inarudi kwa aliyetuma.
Kwa
huduma hii, mteja anapaswa kuchangia huduma ya kutuma pesa kutoka kwa
menu ya kawaida, halafu anachangua kutuma pesa kwenda mitando mingine.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutembelea watumiaji
wa huduma za kutuma na kupokea pesa, Meneja wa Airtel Money kutoka
kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce alisema kupitia muungano wa
Taifa Moja wameweza kuwafanya wateja wapate njia rahisi ya kutuma na
kupokea fedha.
Tunajua
hapo zamani kuna baadhi ya wateja walikuwa wanapata wakati mgumu
linapokuja suala la kutuma na kupokea fedha. Ilikuwa aidha upokee fedha
kwa ujumbe mfupi au uwe na laini ya simu zaidi ya moja. Ukipokea fedha
kwa ujumbe na kwa bahati mbaya ukaufuta ilikuwa inamaanisha fedha
imepotea, alisema Alphonce.
Lakini
vile vile si kila mtu anayepokea fedha kupitia simu ya mkononi
anahitataji kutoa. Wengine wanataka kulipia huduma mbali mbali kupitia
huduma ya simu kama kulipia maji, kununua umeme au matumizi mengineyo.
Kwa huduma hii mpya ya Taifa Moja imekuwa ni njia rahisi kwa wateja
wetu, aliongeza Alphonce
Kupitia
huduma hii ya kutuma pesa na kupokea kutoka mitandao yeyote itachangia
kuongeza idadi ya watu wanaotumia huduma za kutuma na kupokea fedha kwa
kutumia simu za mkononi na pia kuongeza faida kwa makampuni ya simu.
Hii
ni mara ya kwanza Tanzania kwa makampuni ya simu kuungana pamoja kwa
huduma ya pamoja. Hata hivyo, Taifa Moja sio huduma au mtandao mpya
mbali ni njia ambayo imepewa promosheni hii ya kutuma na kupokea fedha
kutoka mtandao wowote.
Kwa
upande wake, Mkuu wa usambazaji mkoa wa Dar es Salaam kutoka kampuni ya
Tigo Tanzania Lloyd Kaaya. alisema ni furaha kwao kuona kwamba wateja
wa simu za mkononi kwa sasa hivi anaweza kutuma na kupokea pesa kutoka
mtandao wowote kwa gharama zile zile. Hii inaamanisha matumizi wa kutuma
pesa yataongeza na yatakuwa na manufaa kwa upande wetu, alisema Kaaya.
No comments:
Post a Comment