Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji
akiba kwa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika
Makao makuu ya Mfuko mjini Dodoma .
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw.
James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu
wa matumizi ya teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia
Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
Meneja mwenye dhamana na Skimu ya uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa ili kuweka
akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
mjini Dodoma.
Afisa huduma kwa wanachama wanaoweka akiba kwa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bw. Juma Venerando akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi Mfuko wa
Pensheni wa LAPF ulivyojipanga kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa wanachama.
Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Mkoani Dodoma Bw. Gideon Morris akizungumza na
waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha
ubora zaidi wa huduma zao za Tigo-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote
kuweka akiba ya hiari Kwenye Mfuko wa LAPF.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Mkoani Dodoma Bw. Balikulije Mchome
akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika
kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za M-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania
wote kuweka akiba ya hiari katika Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo
mbalimbali yaliyotolewa kwenye utambulisho wa huduma za uwekaji wa akiba ya hiari
kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mkutano
uliofanyika mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment