Monday, April 24, 2017

KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION CHAPATA UONGOZI MPYA

 Msimamizi wa uchaguzi kaka Boi Juma akiweka mambo sawa kwa kusoma mwongozo wa zoezi hilo huku msaidizi wake Yusuf  Issa "Jesse" Kimvuli akiwa pembeni
 Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mohamed "Muddy" Irapo akijieleza na kuomba kura.
 Mwenyekiti wa muda aliyemaliza muda wake na mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bw. Mohamed Bhinda akisubiri kujieleza na kuomba kura
 Wanachama wakipiga kura
 Mweka hazina Msaidizi Bakari Simba
 Katibu Mkuu Wahid Abdulghafoor
 Katibu Mkuu Msaidizi Fabian Kimonga
 Msimamizi wa uchaguzi Boi Juma akitoa maelekezo

 Kura za wanachama walio nje ya nchi zikihesabiwa
 Iddi Ushiro akirusha zoezi hilo mubashara ambapo walio nje ya nchi wote waliona na kushiriki kikamilifu
  Kura za wanachama walio nje ya nchi zikiendelea kuhesabiwa
 Bakari Simba akigawa biskuti baada ya zoezi la kupiga kura
 Mjumbe Idrissa Jumbe akishukuru kwa uchaguzi huru na wa haki
 Mjumbe Salma King akishukuru kwa kuchaguliwa
 Mwenhyekiti mpya wa KFDF Alkareem Bhanji akipongezwa
 Msimamizi wa uchaguzi akipata picha ya pamoja na wanachama
 Msimamizi wa uchaguzi akipata picha ya pamoja na wanachama
 Msimamizi wa uchaguzi akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF


MATOKEO RASMI  YA UCHAGUZI WA KFDF TAREHE  23/4/2017 DAR ES SALAAM
Wanachama halali na hai walioshiriki uchaguzi  mkuu wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) uliofanyika siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam ni 41, ambapo wanachama 23 walikuwepo ukumbini na wanachama 18 waishio nje ya nchi walipiga kura kwa njia ya mtandao. 

Nafasi ya Mwenyekiti

1.Alkarim Bhanji alipata;
 Kura za ndani 23
 Za nje               16
Jumla 39.
Mshindi Ni Alkarim Bhanji

2.Makamu Mwenyekiti


Mohammed Bhinda amepata kura;
  Za  ndani 9
   Za  nje     5
Jumla 14.

Mohammed Irapo amepata kura;
Za ndani 14
 Za nje 11
Jumla 25
Mshindi kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Mohammed Irapo

3.Mweka Hazina msaidizi.

Za ndani 23
Za nje 15
Jumla 38

Bakari Simba ameshinda kwa kupata kura;

4. Katibu Mkuu 

Za ndani 23
Za nje   15
Jumla 38

Wahid Abdulghafoor ameshinda nafasi ya 
katibu mkuu

5. Katibu Mkuu Msaidizi
Za ndani 23
Za nje 14
Jumla 37

Fabian Kimonga ameshinda  nafasi ya katibu Msaidizi 

6. Wajumbe

Wajumbe walichaguliwa kwa kupata kura 37 kila mmoja.
Majina ya wajumbe waliochaguliwa ni;
1.Shaaban kessy
2.Abdallah kizua
3.Idrissa Jumbe
4.Sophia Muccadam
5.Salma King

Nafasi mbili ambazo hazikugombewa ni Mweka Hazina na Mjumbe Mmoja ambapo inalazimika kufanyika kwa uchaguzi mdogo. Pia kwa mujibu wa katiba inatulazimu kuwateua rasmi Mkuu wa mawasiliano na msaidizi wake ,ambao nafasi zao zilikuwa si za kugombaniwa isipokuwa ni za kuteuliwa.


Uongozi unapenda kutoa shukrani za dhati kwa msimamizi wa uchaguzi, kaka yetu Boi Juma, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Klabu ya Saigon, kwa kusimamia zoezi zima kwa weledi wa hali ya juu.

Imeandaliwa na: 
Wahid Abdulghafoor
Katibu Mkuu KFDF

No comments: