Na Freddy Macha
Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.
WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya.
Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.
Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton.
Furaha na shangwe ya WASATU
Balozi Migiro (katikati) na mwana WASATU- mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde
Muziki motomoto, Northampton
Bango la shughuli
Balozi Migiro akihutubia tafrija
Mpiga sasafoni mkongwe na mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz
WASATU. Toka kushoto nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha
Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya. Picha na Shah
Vitumbua vya Neema Kitilya
Nyama Choma
Mwana WASATU Fab Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi
Mwanamuziki wa Kikongo aliyehamia Tanzania miaka mingi, Kawele Mutimanwa na bendi ya “Afrika Jambo” jukwaani Northampton
Mwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka Kenya aliyetengeneza tangazo la WASATU
Mwanamuziki wa Kikongo Mboka Lia ( anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”) ndani ya nyuzi na sakata sakata la WASATU
Mwanamuziki mlemavu aliyekomaa- mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana WASATU aliyebobea. Kileleni Northampton bila kukosa.
No comments:
Post a Comment