Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akikabidhi zawadi kwa
mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tewe iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na ya
sita kimkoa
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji Bw William
Makufwe wakisomewa namba na wanafunzi wa shule ya awali kabuku nje
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji
wakisikiliza mwanafunzi alipokuwa akielezea tense za somo la kiingereza
wanafunzi wa shule ya sekondari kabuku akielezea mifumo ya kibaiolojia Kwa viongozi
Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza wakati wa Hafla hiyo
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe wakatikati na Mkurugenzi Mtendaji
Bw William Makufwe wa mwisho kulia na kaimu afisa Elimu Msingi Bw
Fikeni senzige wakikagua gwaride la wanafunzi wa kabuku.
mwalimu na wanafunzi wkisherehesha Hafla hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye
mitihani ya darasa la saba na kidato cha
nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la
elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku
nje.
Akizungumza kwenye maadhimisho
hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin
Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya
na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
“elimu ni ufunguo wa maisha na
kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni watoto kutumia fursa ya Elimu bure
inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.
Aidha ameeleza kuwa atahakikisha
fedha zinazohusu madai ya walimu
zinapofika Halmashauri zinawafikia
walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata
kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.
Wakati huohuo amepiga marufuku
watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuacha kuchunga mifugo hasa kwa siku za
shule baada ya kubainika watoto wengi wa jamii ya wafugaji wanatumiwa kuchunga
mifugo badala ya kwenda shule.
Amewaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao
wanakwamisha watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria
itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume. Amewaeleza pia wazazi
ambao wanawatoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji Bw. William Makufwe ,amesema kuwa
kukosekana kwa chakula cha kutosha shuleni,utoro uliokithiri kwa baadhi
ya wanafunzi,kutokuwajibika kwa baadhi ya walimu na wazazi pamoja na upungufu
wa walimu kunasababisha kwa kiwango kikubwa kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.
Ameagiza shule ambazo mpaka sasa
ambazo hazina chakula kuhakikisha wanawapa wanafunzi chakula. Aliwataka pia kusimamia mazao ya
mihogo waliyopanda ili mazao hayo yaweze kusaidia upatikanaji wa chakula
shuleni na kuongeza kiwango cha uelewa
kwa wanafunzi.
Ametoa mwezi mmoja hadi kufikia 4/5/2016 kwa Maafisa watendaji Kata,
Vijiji, walimu wakuu, wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kuhakikisha kuwa
watoto wanapata chakula cha mchana shuleni.
Shule za Msingi zilizopata zawadi
na pongezi ni Tewe iliyokuwa ya sita kimkoa na kuzawadiwa Tsh. 200,000/=.,
Chang’ombe Tsh. 150,000/=, Mkumba Tsh 100,000/=, Mzundu Tsh. 82,000/=,
Kwaragulu , Mbwewe, Kwamdani, Kwedikwazu Magharibi, Kwedikwazu Mashariki na
chogo ambazo zote zilipata Tsh 78,000/=. Mazingara sekondari imepata zawadi
Tsh.100000/=.
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni.
No comments:
Post a Comment