Monday, April 3, 2017

CHUO CHA MICHEZO MALYA KUWA CHA MFANO



Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe akisalimiana na waalimu na viongozi wa Chuo cha Waalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kikazi na kushiriki mahafali ya Chuo hicho na kutoa vyeti kwa wahitimu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt Harrison George Mwakyembe akizungumza katika mahafali ya Chuo cha waalimu Michezo Malya Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw. Yusufu Omary Singo akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi fupi ya uwalimu wa michezo yaliyofanyika Chuo cha Mwaalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza.

Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa kozi fupi ya uwaalimu wa michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe alipokuwa akizungumza nao katika mahafali ya Chuo hicho Jijini Mwanza.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM

…………………………………………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu -Mwanza

Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na hata nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo.

Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe.

Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali, umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu.

Mbali na jukumu la kuongeza aina ya kozi zitakazo tolewa na chuo hicho kwa ngazi ya Stashahada (Diploma) mkuu huyo amemweleza waziri changamoto zinazo kikabili chuo hicho ambazo nipamoja na uhaba wa maji, Gym ya mazoezi, hali inayosababisha timu mbali mbali za mpira wa miguu zinazo tamani kwenda kuweka kambi katika eneo hilo kushindwa kutokana na ukosefu wa Gym, “Mh. Waziri ilikuja timu ya Mbao FC, kilio chao kikubwa ilikuwa ni eneo la Mazoezi ya viungo (Gym Fitness centre)” alisema mkuu huyo wa chuo.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Michezo nchini Dkt. Yusuph Singo Omary, kutoka Wizara ya habari, amesema hivi sasa Serikali ipo katika mchakato wa kutenga shule 55 ikiwa ni hatua itakayo saidia katika kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini kuanzia vijana wanapokuwa wadogo.

Awali akimkaribisha Waziri wa habarikuzungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi Msafiri, alimuomba waziri, Wizara ya habari kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kuona Umuhimu wakukisaidia chuo hicho katika kukiendeleza, “Tunaomba Mhe. Waziri ili chuo hiki kiweze kwenda mbele basi vema kila Halmashauri ikaagizwa kugharamia angalau Walimu wawili kila mwaka”, alisema Msafiri na kuongeza kuwa endapo Halmashauri zote nchini 189, zikileta walimu wawili tu basi tutakuwa na wanafunzi 378, hii itakisaidia chuo chetu kukua zaidi, lakini pia kupata walimu wenye weledi.

Kwa upande wao wahitimu hao wamemuomba waziri kupewa kipaumbele katika Michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA, Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Catherine Laurent, amesema wao wamejifunza Sheria na kanuni za Michezo mbali mbali kwa kipindi chote walichokuwepo chuoni hapo hivyo wanaomba kupewa kipaumbele katika kufundisha michezo pindi warejeapo kwenye vituo vyao vya kazi kwani sasa wanatambua sheria, kanuni na taratibu zinazo ongoza michezo waliyo jifunza.

Chuo cha michezo Malya kilianzishwa mwaka 1979, kikiwa na lengo la kufundisha na uendeleza walimu wa michezo katika ngazi ya Astashahada na badae mwaka 1995, ndipo kilianza kuzalisha walimu wanafunzi wa ngazi ya Stashahada (Diploma). Lakini pia kimekuwa kikiendesha kozi fupi za wiki mbili ambazo huwajengea uwezo wahusika kabla yakuendelea na ngazi ya Diploma.

No comments: