Na MatukiodaimaBlog
ASKOFU mkuu wa kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Dkt Rejoice Ndalima amewataka viongozi wa dini nchini kutumia nyumba za ibada kumwombea Rais Dkt John Magufuli na kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba hizo kusema kuumbua viongozi wa serikali.
Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika nchi hii si ya kubenzwa makanisani na wachunguzaji ama viongozi wengine wa dini bali ni kazi ambayo inapaswa kuombewa zaidi ili Taifa lizidi kubarikiwa.
Askofu huyo ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo Mtwivila mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul Mtakwimwa ,kuwa hivi sasa heshima ya nyumba za ibada imeanza kupoteza uwepo wa Mungu kutokana na baadhi ya watu kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya masengenyo na utapeli jambo ambalo si sahihi.
Alisema kitendo cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya watu kuishambulia serikali ama kufanya utapeli wa fedha za waumini wao kwa kuwatoza fedha kama malipo ya huduma wanayoitoa si sahihi na si kazi ya nyumba za ibada hasa makanisa.
Pasipo kutaja majina ya makanisa yaliyogeuzwa majukwaa ya wanasiasa na baadhi ya watu waovu ama yanayofanya utapeli wa pesa kwa waumini wake ,alisema kuwa yamezuka makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa kuitwa makanisa ili yalipaswa kuwa ni vyama vya siasa ama nyumba za waganga wa kienyeji kwa maana ya wapiga ramli.
“ Baadhi ya makanisa yamepoteza sifa ya kuitwa ni makanisa maana wanafanya vituko vya ajabu sana ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo wanaotumiwa na wanasiasa kueneza siasa makanisani na kila siku wao ni kuwa ni wachonganishi dhidi ya serikali na watu wake na wengine wamegeuka watabiri wa uongo na watenda miujuzi hatarishi kwa jamii “
Alisema kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kuhubiri neon ili watu wote waweze kumjua Mungu na sio kuhubiri siasa ama kuifundisha kazi serikali ya kufanywa wakati si jukumu la kanisa kuwa iwapo watu wote watamjua Mungu watafanya kazi ya kuhudumia jamii kwa kutanguliza hofu ya Mungu hivyo hakutakuwa na ufisadi , wizi ama watumishi hewa hivyo kazi ya kanisa ni kuwafanya watu waijue kweli na kweli iwe ndani ya mioyo yao.
Askofu Dkt Ndalima alisema kuwa kanisa lake limeenea nchi nzima na katika mkoa wa Iringa wameanzisha makanisa mawili katika mji wa Iringa na Nyololo wilaya ya Mufindi ila lengo lao ni kuhubiri neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa kanisa la ujanja ujanja kama wanavyofanywa baadhi ya watu wanaojiita manabii ila kazi wanayoifanya ni sawa na manabii wa uongo .
Akielezea kuhusu utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli askofu huyo alisema kanisa lake linampongeza kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna tena maandamano ya vurugu na kuwa kila wakati makanisa yake yatatenga mudu wa kumuombea Rais na watendaji wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada zake na sio kutumia matukio na kashfa za viongozi kuhubiri kanisani.
|
No comments:
Post a Comment