Saturday, March 18, 2017

WAMILIKI WA HOTELI MKOANI MBEYA WAASWA KUAJILI WAHUDUMU WENYE SIFA




Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya jumla ya wahitimu 74 waliopewa mafunzo ya siku tatu katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST Mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia)
Baadhi ya wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.

Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii,Jesca William akiwaonesha baadhi ya video zinazotumika katika kutoa mafunzo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu.
Mmoja wa Wahitimu wa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu, Lyimo Leb akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi kabla ya mafunzo hayo kufungwa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akizungumza na wahitimu kabla ya kufunga jana mafunzo hayo fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya wahitimu 74. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru (kulia)

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa wenye hoteli katika mkoa wa Mbeya, Jeremiah Mchange cha ushiriki wa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi
Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru akizungumza na wahitimu kabla ya kufungwa mafunzo hayo jana katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74. (Picha na Lusungu Helela- WMU)

…………………..

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi amewataka wamiliki wa hoteli kuajiri wafanyakazi wenye ujuzi katika fani ya ukarimu na utalii baadala ya kuajiri ndugu zao wasio na ujuzi wowote na kuwalipa ujira mdogo hali inayochangia kuzorotesha huduma za utalii mkoani hapo.

Alisema wahudumu walio wengi katika hoteli hizo wamekuwa kero katika utoaji wa huduma kwa watalii pindi wanapotembelea kuja kuona vivutio vya utalii vilivyopo mkoani hapo.

Ametoa raia hiyo jana wakati akifunga mafunzo hayo kwa jumla ya wahitimu 74 yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Amesema Wahitimu hao wamepewa mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi kwa ufadhili wa asilimia 75 uliofanywa kupitia mradi wa SPANEST

Aidha, Mushi alisema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii tayari umejipanga katika kuboresha sekta ya utalii ambapo kwa mkoa wa Mbeya imeshaandaa Mpango Mkakati wa kuendeleza utalii .

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwa wahudumu na pamoja na wamiliki wa hoteli ili waweze kutambua umuhimu wa wafanyakazi wao.

Naye, Mratibu wa Mradi wa SPANEST, Godwell Mengiaediek amewataka wahudumu wa hoteli waunde chama chao ambacho kitawasaidia katika kupaza sauti zao.

No comments: