Thursday, March 16, 2017

WALENGWA WA TASAF WILAYANI KILOMBERO WAITIKIA WITO WA SERIKALI WA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO KWA FEDHA ZA RUZUKU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI.


NA ESTOM SANGA-TASAF.

Wahenga walinena ‘’mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe’’na ‘’penye nia pana njia’’ni semi zilizoanza kuonekana kwa vitendo miongoni mwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Baadhi ya walengwa wa Mpango huo wameanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mafuta ya mawese kwa kutumia fedha za ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia TASAF.

‘’ Baada ya kupata fedha za TASAF niliamua kununua mbegu za mawese na kisha kuanza kuzisindika kwa lengo la kukamua mafuta ya mawese na hadi sasa nimepiga hatua ya kujivunia’’ ninaishukuru sana serikali na TASAF amesema bi.Coletha Emilliani Nipala mkazi wa eneo la Mbasa katika mji wa Ifakara.

Anasema mbali ya changamoto ya udogo wa mtaji hajakumbana na tatizo la soko kwani mafuta ya mawese yanahitajika kwa kiwango kikubwa kwa matumizi ya walaji na hata kutengenezea sabuni.

Walengwa wengine pia wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali ikiwemo ufugaji wa nguruwe, mbuzi kuku, na hata kuanzisha migahawa midogo midogo inayowaongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

Walengwa waliotembelewa na Waandishi wa Habari wameeleza kuwa hali zao za maisha zimeboreshwa baada ya kuingizwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watoto wao kuhudhuria masomo ambalo ni mojawapo ya masharti ya Mpango.

Zifuatazo ni picha za baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kilombero wakinyesha mafanikio yao.
Bi.Lucia Ngalota (aliyevaa kitambaa kichwani) mkazi wa kijiji cha chita wilaya ya Kilombero akiwaonyesha waandishi makazi yake mpya aliyoijenga baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF.
Hii ni nyumba aliyokuwa akiishi bi Lucia kabla ya kuorodheshwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambayo imeanza kubomoka.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini B.Stela Samson Samusam- mkazi wa kijiji cha Chita akiwa nje ya nyumba aliyoijengwa kwa fedha za Mpango unaotekelezwa na TASAF.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini B.Stela Samson Samusam- mkazi wa kijiji cha Chita akiwa nje ya nyumba aliyoijengwa kwa fedha za Mpango unaotekelezwa na TASAF.
Mmoja wa walengwa wa TASAF Bi.Mchilo Omary Kibwana mkazi wa kijiji cha mchombe akiwa katika mgahawa wake aliouanzisha kwa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.Picha ya chini ni nyumba aliyoijenga kutokana na faida aliyoipata kupitia mpango huo.
Mmoja wa walengwa wa TASAF Bi.Mchilo Omary Kibwana mkazi wa kijiji cha mchombe akiwa katika mgahawa wake aliouanzisha kwa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.Picha ya chini ni nyumba aliyoijenga kutokana na faida aliyoipata kupitia mpango huo.
Nguruwe wanaofugwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo la Mbasa wilaya ya Kilombero kama njia mojwapo ya kujiongezea kipato.
Nyumba ya walimu iliyojengwa TASAF kupunguza tatizo la makazikwa walimu katika shule ya msingi Mbasa shule anbayo pia kuna wanafunzi kutoka kaya za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini.
Mbali na kutoa ruzuku kwa walengwa, TASAF pia imeendelea kujenga majengo ya shule na nyumba za walimu kama anathibitisha Mkuu wa Shule ya msingi Mbasa katika wilaya ya Kilombero Mwl. Aman Ngowi akihojiwa na waandishi wa habari juu ya ujenzi wa nyumba inayoonekana nyumba yake.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Mbasa wilaya ya Kilombero Bi. Coletha Emilian Nipala (aliyevaa kitambaa chekundu kichwani) akihojiwa na Waandishi wa Habari namna alivyoweza kutumia fedha zaruzuku kutoka TASAF kuanzisha kiwanda kidogo cha kusindika mawese na kujiongezea kipato.Picha ya chini ni mbuzi anaowafuga baada ya kununua kwa ruzuku kutoka TASAF.
Bi. Victoria Johnson Nguge mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Chita akihojiwa na Waandishi wa Habari juu ya mafanikio aliyoyapata tangu aorodheshwe kwenye Mpango ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba.

No comments: