Monday, March 6, 2017

VIVUTIO VYA UTALII TANGU ENZI ZA MKOLONI VILIVYOPO SHULE YA SEKONDARI YA IYUNGA JIJINI MBEYA

Kamati ya Utalii ya Jiji la Mbeya iliyopo chini ya Halmashauri ya Jiji kupitia kwa Afisa Utalii Bi.Levina Modest jana ilifanya ziara ya kuitembelea Shule ya Sekondari Iyunga iliyopo Mkoani hapo kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa masuala ya Utalii Jijini Mbeya, Uyole Cultural Tourism Enterprises chini ya Mratibu wake Amos Mwamugobole na Asasi nyingine isiyo ya kiserikali iitwayo ELIMISHA chini ya Mkurugenzi wake Bw.Festo Sikagonamo.
Katika Ziara hiyo wajumbe wa Kamati walionyeshwa Vitu mbalimbali vilivyotengenezwa toka enzi za  Mkoloni Mjerumani. Akiongea kwa bashasha kuu Mwalimu mwandamizi wa Michezo,Habari na Utamaduni Sekondari ya Iyunga, Mwalimu Emmanuel Michael ameelezea kwa marefu kuhusu kumbukumbu za kale zilizopo shuleni hapo ikiwemo kengere ya kale,birika,bwawa la kuogelea,mahandaki kwa ajili ya ulinzi,kiti cha kukaa cha kale,matanki ya maji pamoja na majengo vyote vikiwa vilitengenezwa mnamo mwaka 1925.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Utalii ,ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili amemuomba Mwalimu Michael kwa niaba ya Uongozi wa Shule hiyo kushirikiana na Kamati hiyo ili kupata Wazee wa zamani waiishio maeneo hayo ili waweze kupata historia nyingine nyingi kuhusu Utawala wa Kikoloni na taarifa zingine za kina.
Naye Afisa Utalii Bi.Levina amesema kuna kila sababu ya kuboresha mazingira ya Shule hiyo ili yawe ya Kitalii zaidi kwani yataisaidia Halmashauri kujitangaza na kujiingizia mapato huku Shule na wanajamii wa Sekondari ya Iyunga watanufaika pia kwa kuwa na Vivutio hivyo.
Mwishowe,Mwalimu Emmanuel Michael aliushukuru Uongozi wa Halmashauri ,Kamati ya Utalii kwa kuliona suala la Utalii kuwa ni jema na kuamua kulishupalia na kuiahidi Kamati hiyo kushirikiana nayo bega kwa bega katika kufanikisha suala hilo zuri huku akiiomba Kamati utekelezaji mwema wa majukumu yake.

Kiti hiki cha kukalia ni moja ya kivutio shuleni hapo kilitengenezwa zaidi ya miaka 90 iliyopita enzi za Utawala wa Kikoloni wa Kijerumani

Ukuta huu ulijengwa na Wajerumani pembezoni mwa Mto Nzovwe kwa ajili ya Ulinzi na Usalama kwani chini ya Ukuta huu kuna Handaki kubwa linalounganisha maeneo ya ndani ya shule na nje ya eneo hilo

Hili ni birika la kale lililokuwa likitumika na Utawala wa Kijerumani kwa ajili ya kuhifadhia maji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo ambalo Uongozi wa Shule ya Sekondari Iyunga wamelitunza vizuri hadi hivi sasa

Hiki ni kifaa kitumikacho Kuratibu masuala mbalimbali kuhusu Hali ya Hewa (Stevenson Screen) kilichojengwa na kutumika tangu enzi za mkoloni Mjerumani

Jengo hili ni Ukumbi uliojengwa na Mkoloni ambao ndani yake kuna Handaki linalotoka mpaka nje ya maeneo ya Shule hiyo, Juu kulia karibu na dirisha ni Kengere ya Mkoloni inayotumia umeme iliyokuwa ikitumika kutoa taarifa mbalimbali kama kuna hatari au kuita watu mkutanoni kwa ajili ya kujuzwa yanayojiri

Kamati ya Utalii ya Jiji, Waandishi wa Habari pamoja na Mwalimu mwenyeji Mwl Emmanuel Michael wakiwa eneo lilipo Bwawa la Kuogelea lililojengwa na Enzi za Mkoloni

Afisa Habari wa Halmshauri ya Jiji la Mbeya Bi.Jacqueline Msuya akitoka ndani ya Handaki pamoja na wajumbe wengine waliokuwa wakizungukia maeneo ya utalii ndani ya Shule ya Sekondari ya Iyunga,Jijini Mbeya

Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii na Diwani wa Kata ya Sisimba Mhe.Geofrey Kajigili (wa kwanza kushoto) akiwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mwenyeji wao Mwalimu Emmanuel Michael wa Sekondari ya Iyunga

Mwalimu Emmanuel Michael ,Mwalimu mwandamizi wa Michezo,Habari na Utamaduni akielekeza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Utalii ndani ya Handaki lililopo shuleni hapo
PICHA YA PAMOJA: Wajumbe wa Kamati, Waandishi wa Habari na Mwalimu mwenyeji kwenye viunga vya Shule ya Sekondari Iyunga

Wajumbe wa Kamati ya Utalii wakifurahia mara baada ya Kuelezwa mambo mbalimbali na kuyatembelea, hapa wakiwa kwenye pozi la kuruka juu ndani ya Bwawa la Kuogelea lillilojengwa tangu Enzi za Mkoloni miaka 90 iliyopita
FADHIRI ATICK 01:36 (2 hours ago) to me
Kamati ya Utalii ya Jiji la Mbeya iliyopo chini ya Halmashauri ya Jiji kupitia kwa Afisa Utalii Bi.Levina Modest jana ilifanya ziara ya kitalii kuitembelea Shule ya Sekondari Iyunga iliyopo Mkoani hapo kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa masuala ya Utalii Jijini Mbeya, Uyole Cultural Tourism Enterprises chini ya Mratibu wake Amos Mwamugobole na Asasi nyingine isiyo ya kiserikali iitwayo ELIMISHA chini ya Mkurugenzi wake Bw.Festo Sikagonamo.

No comments: