Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Vikundi mbalimbali vya Jogging viliweza kufanya mazoezi kwa pamoja kwa mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa na kumalizikia viwanja vya Mwembe Yanga na kuhamasisha ushirikiano baina yao.
Mbio hizo zilizofanyika jana, vilikutanisha vikundi zaidi ya 15 kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Temeke pamoja na baadhi kutoka wilaya ya Kinondoni ikiwa ni kuunga mkono katila jitihada za ushirikiano baina yao.
Mwenyeji wa Mbio hizo Kikundi cha Dar Jogging kutoka maeneo ya Chang'ombe kiliwaalika vikundi vingine ikiwa ni moja ya malengo ya kujenga ushirikiano baina yao ikiwemo kujihusisha na masuala ya upatu (saccoss).
Mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo ujulikanao kama Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia amesema kuwa vikundi hivyo vinatakiwa kushirikiana kwa njia mbalimbali ili kuweza kujiwezesha kiuchumi na zaidi kuanzishwa kwa upatu baina yao ni mwanzo mzuri wa maendeleo.
Amesema kuwa, kuanzishwa kwa upatu baina ya vikundi ni moja ya malengo chanya katika kujiinua kiuchumi na kuweza kuanzisha miradi mbalimbali itakayokuwa inasimamiwa na wana vikundi hao ambapo amewapongeza Dar Jogging kwa hatua waliyofikia.
Naye Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka amewashukuru vikundi vya Jogging vilivyokubali mwaliko wao na zaidi amewataka kushirikiana kwa pamoja kuona wanatafuta ufumbuzi wa masuala yanayowakabili hususani kwenye vikundi mbalimbali na changamoto wanazokutana nazo.
Namkoveka ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea (TSA) amesema katika fedha walizozipokea za Upatu takribani kiasi cha shilingi laki saba (700,000) watahakikisha wanazifanyia malengo waliyoyapangia ikiwemo kuhitaji kununua boda boda za kufanyia biashara.
Mwenyekiti wa umoja wa vikundi Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia akizungumza na wanajogging waliojitoeza katika mbio hizo zikiwa na malengo ya kuhamasisha ushirikiano baina yao na kujitafutia njia za kujiinua kiuchumi jana kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga.
Mwenyekiti wa umoja wa vikundi Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia akikabidhi pesa taslimu kiasi cha shillingi laki sabai (700,000) zilizopatikana katika mchezo wa upatu unaochezwa na vikundi hivyo vya Jogging akishuhudiwa na wajumbe wengine kutoka umoja wa vikundi hivyo. Wanachama wa kikundi cha Dar Jogging wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mbio hizo.
No comments:
Post a Comment