Na Mboza
Lwandiko
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imeshiriki Mkutano wa mwaka wa 18 wa
Benki ya Dunia unaohusu masuala ya Ardhi na Umaskini, Machi 20 – 24, 2017 –
Washington DC – Marekani.
Mkutano
huo unaobeba ujumbe; “Utawala bora wa Ardhi”, umejumuisha zaidi ya wajumbe
1,200 kutoka nchi wanachama, zilizohusisha Serikali, taaluma, jamii na Sekta
binafsi mbalimbali.
Pamoja
na mambo mengine; Mkutano huo umejikita zaidi katika Maboresho mbalimbali
yanayoendelea kufanyika katika Sekta ya Ardhi Duniani, ikiwa ni pamoja na
kuzingatia nafasi ya takwimu na shuhuda zinazoashiria maboresho katika Sera za
Ardhi, na kuainisha Mikakati ya Maendeleo katika kuboresha zaidi Sekta ya
Ardhi.
Aidha,
Mada ambayo imewasilishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
imewasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara; Dkt. Yamungu Kayandabila, ambayo
ilibeba ujumbe - “Ardhi; Ufunguo wa
Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa Tanzania”. Alieleza kuwa utawala wa
Ardhi Tanzania unazingatia; Sheria, Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa
Wananchi. Pamoja na mengine Dkt. Kayandabila alieleza jitihada mbalimbali
ambazo zimekuwa zikifanyika kuboresha sekta ya ardhi nchini na juhudi ambazo
zinaendelea kuboresha utawala bora wa Ardhi nchini.
Baadhi
ya maboresho aliyoyataja ni pamoja na; Kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya
mwaka 1995, Upimaji wa viwanja katika maeneo ya vijijini; mfano; Ulanga,
Kilombero na Mvomero (Morogoro) kwa mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha
Ardhi (LTSP) na uendeleaji wa kujenga mfumo unganishi wa taarifa za ardhi
ujulikanao kama Integrated Land
Management Information System (ILMIS).
Wajumbe
wengine waliohudhuria Mkutano huo ni pamoja na; Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango
na Matumizi ya Ardhi (NLUPC),
Dkt. Stephen Nindi, Kamishna msaidizi wa Ardhi, kanda ya Dar es Salaam; Mathew
Nhone; Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji; Immaculate
Senje, Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ; Amina Rashidi,
wote wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni; Aaron Kagurumjuli na Afisa Ardhi wa Manispaa ya
Kinondoni; Rehema Mwinuka.
Aidha,
ujumbe kutoka Tanzania ulipata fursa ya kuonana na ujumbe wa Finland akiwemo aliyekuwa balozi wa zamani wa Finland
nchini Tanzania; Sinikka Antila, Mkurugenzi wa upimaji na ramani wa Finland na
wawakilishi wa makampuni mbalimbali ya vifaa vya upimaji na ramani na softwares wa Master plans. Wajumbe hao walifikia makubaliano ya ujumbe wa Finland
kufika Tanzania kwa mazungumzo zaidi.
Baadhi
ya mada zilizowasilishwa kwenye Mkutano huo ni; Jinsi utawala wa ardhi,
unavyoongeza kodi ya Mapato na kuwezesha upatikanaji wa Ajira, Worldbank, Uganda; Matumizi ya takwimu
za ardhi kwa utawala wa Serikali za Mitaa. Location
International; UK ; Kuboresha Utawala wa Ardhi kwa Utawala Bora; Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijji, Uganda; Kuwezeshwa kwa Wananchi na
Matumizi ya Ardhi, maendeleo ya ardhi na utawala wa taasisi, Kenya; na Uzoefu
wa Sekta Binafsi katika sekta ya Ardhi- USAID,
Marekani.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi
No comments:
Post a Comment