Tuesday, March 28, 2017

STAR TIMES YAZINDUA KAPU LA PASAKA

Maeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino akizungumza waandishi wa habari

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni ya kuuza Ving’amuzi ya StarTimes Tanzania inatoa pakacha la pasaka  kwa wateja wake ambapo kampuni hiyo imetangaza kuwa kuanzia tarehe 16 Machi 2017  wateja watakaojiunga na kifurushi cha kuanzia Mambo watapata ofa ya wiki moja  ya kifurushi cha Uhuru.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo Maeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino amesema kuwa wateja waliolipia  watafurahia maudhui mazuri yatakayokidhi na kuburudisha familia msimu mzima  wa pasaka.Ambapo ndani ya wiki nne (4) wiki moja ya kwanza mteja atafurahia kifurushi cha juu.
“ Watazamaji watakaolipia mwezi moja kifurushi cha Mambo (sh.12000) wataweza kufuruhia wiki moja kifurushi cha Uhuru (sh.24,000) ambayo inazaidi ya chaneli kumi na tano (15). Chaneli hizo ni pamoja na Startimes Novella, ,Nat Geo Wild,Startimes World Football,Sport Arena  na Nyingine Nyingi”. Amesema Awino
 “pakacha la pasaka linatoa fursa nzuri kwa watazamaji kujionea maudhui mazuri yanaopatikana kwenye vifurushi vya Uhuru na Super na pia katika  kifurushi chochote  watakacholipia msimu huu  kwenye kingamuzi cha StarTimes” ameongeza  Awino
Startimes inatoa bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya kingamuzi,televisheni ya kidigitali,simu na huduma ya kulipia kifurushi.Tutaendelea kuwapa wateja huduma za kisasa  na nafuu zinazoendana na wakati kulingana na ukuaji wa teknolojia na mahitaji ya wateja ili kufurahia ulimwengu wa kidigitali.

No comments: