Wednesday, March 8, 2017

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WAZIRI KAIRUKI AONGOZA KUFANYA USAFI MUHIMBILI

Waziri Kairuki (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Muhimbili, Agness
Mtawa. Kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Umoja wa Wanawake katika Wilaya ya Ilala, Joyce Ibrahimu Mkaugala na Zuhura Mawona wakifanya usafi Leo katika hospitali hiyo.
Waziri Kairuki akizungumza na kinamama waliojifungua watoto kabla ya kuwapatia zawadi ya nguo za watoto, pampazi na sabuni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akizungumza na  wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo kabla ya kukabidhi vitanda 10 na magodoro 10 kwa uongozi wa hospitali hiyo. Katika kusherekea siku ya wanawake duniani leo, pia Waziri huyo amewapatia kinamama zawadi mbalimbali zikiwamo nguo za watoto na sabuni. Kushuto Mkurugenzi wa Uunguzi katika hospitali hiyo, Agness Mtawa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akikabidhi vitanda 10 na magodoro 10 kwa Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),Agness Mtawa.
Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akimshukuru Waziri Kairuki baada ya kupokea msaada wa vitanda na magodoro leo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- leo imeungana na wanawake
wengine ulimwenguni kote kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.

Zoezi hilo limeongozwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Dar
es salaam Mheshimiwa Angellah Kairuki kwa niaba ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi –UWT- mkoani humo.

Mheshimiwa Kairuki ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani UWT imeona ni vema wakashiriki
katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuonesha dhamira ya dhati kwamba CCM inawajali wananchi wake bila kujali itikadi ya chama.

‘’ Sisi tumekuja hapa Muhimbili kushiriki na nyinyi katika kuadhimisha
siku hii kwa kufanya usafi bila kujali itikadi ya chama kwani Hospitali hii
inahudumiwa wananchi wote , pia siku hii ya leo tunatoa msaada wa vifaa mbalimbali vya watoto na wenzetu wengine wameenda katika Hospitali
zingine wote tukiwa na lengo moja’’. Amesema Waziri Kairuki.

‘’Msaada tuliotoa ni vitanda kumi, magodoro kumi , mashuka na vifaa vingine mbalimbali vya watoto zikiwamo nguo ,sabuni na Pampers lengo
ni kuunga mkono juhudu za serikali za kuboresha huduma za afya hususani afya ya mama na mtoto na kuhakikisha hakuna mgonjwa anayelala chini kwa kukosa kitanda’’ . Amesema Mheshimiwa Kairuki.

Akipokea msaada wa vitanda hivyo Mkurugenzi wa Huduma za
Uuguzi na Ukunga wa MNH Agnes Mtawa amewashukuru UWT kwa msaada walioutoa ambao amesema umekuja wakati muafaka kwani utasaidia katika kutekeleza majukumu yao .

Hata hivyo Mkurugenzi Mtawa amewakumbusha wauguzi kuendelea
kufanya kazi kwa kufuata maadili na kusisitiza kuwa kazi hiyo inahitaji kujitoa na kuwa na moyo wa huruma .

Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila Machi nane ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’ Tanzania ya Viwanda , Wanawake ndio msingi wa mabadiliko ya kiuchumi .

No comments: