Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira
kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akizungumza katika uzinduzi wa
programu ya kuboresha miundombinu ya usalama wa Barabarani kwa shule za msingi
iliyoanzishwa na Shirika la Amend kwa
kushirikiana naTaasisi za Puma Energy na Fia. Mpango huo uliozinduliwa katika
shule ya msingi Mpakani, Manzese Tip Top
umeanzishwa kwa lengo la kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi kupata
ajali za barabarani.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma
Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa
program ya ujenzi na uboreshaji wa mindombinu ya usalama wa barabarani kwa
shule za msingi. Corsaletti alianisha kuwa usalama barabarani ni ajenda namba
moja kwa kampuni yao na mpaka sasa wamekwisha toa mafunzo ya aina hayo kwa wanafunzi 39,000
kutoka shule 33 mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Geita.
Mkurugenzi
wa Mpango hu wa Shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana akizungumza
katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo akikata
utepe kuzindua mpango wa kuwalinda wanafunzi wa shule za msingi kupatwa na
ajali za Barabarani ulionzishwa na Shirika la Amend kwa msaada wa taasisi ya
Puma Energy na Taasisi ya Fia kwenye shule ya msingi Mpakani ya Manzese Tip
Top. Wengine katika picha ni Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe
Corsaletti (wa tano kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Amend, Ayikai Poswayo (wa
kwanza kulia) na Diwani Kassim Lema ( wa kwanza kushoto).
Washiriki
katika uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye eneo ambalo limetengenezwa
rasmi kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mpakani kuvuka
wakati wa kwenda na kutoka shuleni.
Afisa
Mnadhimu wa Jeshi la Polisi, Thabitha
Makaranga akizungumza katika hafla hiyo. Makaranga aliwamwakilisha
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed
Mpiga.
Wakufunzi
wa masuala ya usalama barabarani kutoka shirika la Amend na wanafunzi wa Shule
ya Msingi Mpakani iliyopo Manzese Tip Top wakionyesha kwa mfano njia sahihi ya kuvuka
barabara.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi 10 zitakazofaidika na mpango wa kuwakinga
wanafunzi wa shule za msingi kupata ajali za barabarani ulioanzishwa na
shirika la kimataifa la Amend kwa msaada mkubwa wa taasisi ya FIA
Foundation na Puma Energy Foundation.
Mpango huo ulizinduliwa juzi kwenye shule ya msingi mpakani iliyopo Manzese Tip Top ambao lengo kubwa ni kujenga miundombinu itakyosaidia wanafunzi kuepuka ajali za barabarani waendapo, wakati wa kuvuka na kurejea kutoka shuleni.
Nchi nyingine ni Benin, Botswana, Ivory Coaste, Ghana, Malawi, Mozambique, Namibia, Senegal na Zambia.
Mkurugenzi wa mpango huo kutoka shirika la Amend, Ayikai Poswayo kutoka Ghana alisema kuwa takwimu si nzuri kwa Tanzania kuhusiana na ajali za barabarani ambapo inakadiliwa kuwa jumla ya watu 16,000 upoteza maisha kutokana na ajali hizo kila mwaka.
Poswayo alisema kuwa kutokana na taasisi yao kujishughulisha na masuala ya usalama wa barabarani katika bara la Afrika, waliamua kuzindua mpango huo hapa nchini kwa lengo la kuwalinda wanafunzi na watu wengine wanaotumia barabara wakati wa shughuli zao za kila siku.
Alifafanua kuwa mpango huo utahusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambayo itatumiwa na watembea kwa miguu, waendesha pikipiki, baiskeli na magari kuepuka ajali hizo ambazo nyingi zimeleta madhara kwa watu na wenginekubakia na ulemavu kama si kupoteza maisha.
“Huu ni mradi wa miaka miwili ambao malengo yake makubwa ni kuwakinga wanafunzi kwenye ajali za barabarani, takwimu siyo nzuri kwa Tanzania, hivyo tumeamua kuanzia hapa na baadaye unzinduzi kama huu kufanyika nchi nyingine, tutajenga miundombinu amayo itawafanya madereva wa vyombo vya moto kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa wastani, mradi huu utafanyika kwenye shule zote zilizopo karibu na barabara,” alisema Poswayo.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti alisema kuwa wanawajibika katika mpango huo kwani ni sehemu ya shughuli zao za kijamii.
Corsaletti alisema kuwa usalama barabarani ni ajenda namba moja kwao na mpaka sasa wameweza kutoa mafunzo ya aina hayo kwa wanafunzi 39,000 kutoka shule 33 mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam na Geita.
Corsaletti alisema kuwa wanafunzi wengi wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha au kupata ulemavu kutokana na ajali ambazo zinatokana na uendeshaji mbaya wa madereva au kukosekana kwa miundombinu ambayo sahihi kuwawezesha wanafunzi kuona kabla ya kuvuka barabara.
Mkurugenzi wwa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Kazi, Injinia Julius Chambo aliipongeza Shirika la Amend, Puma Energy na Taasisi ya Fia kwa kuanzisha mpango huo ili kuwakinga wanafunzi wa shule za msingi.
Injinia Chambo alisema kuwa takwimu za mwaka 2015 za ajali ya barabarani zinaonyesha kuwa zinaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 78 walipoteza maisha kwa mkoa wa Dar es Salaam kutokana na ajali za barabarani. Pia jumla ya watu wanafunzi 182 walijeruhiwa.
“Hali si nzuri, napongeza juhudi za wadau zinazolenga kupunguza ajali za barabarani, kuna makampuni mengi ambayo hayajihuishi na shughuli kama hizi, naziomba ziunge mkono sasa ili kuboresha miundombinu na kuepusha maisha ya wanafunzi,” alisema Chambo.
Alisema kuwa serikali inaiunga mkono juhudi za Puma Energy, taasisi ya Fia na Amend na ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuondoa tatizo hili.
Mwisho…
No comments:
Post a Comment