Tuesday, March 7, 2017

Serikali Yaahidi kushirikiana na vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya Viwanda

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Serikali imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kwa pamoja kuweza kuhamasisha, kuunda na kujenga nchi ya viwanda katika kuunga mkono azma ya Rais Mhe. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na wamiliki na watendaji waandamizi wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhe. Nnauye amesema kuwa serikali na vyombo vya habari wakishirikiana na kuwa na lengo moja wataweza kuileta Tanzania pamoja na kuiweka katika mwelekeo ulio sahihi. 

“Tukiamua leo kila chombo cha habari kikawa na dawati maalumu linalozungumzia Tanzania ya viwanda kama ilivyo kwa madawati mengine ndani ya vyombo vyetu vya habari, na serikali ikaendelea kutoa hamasa za uanzilishwaji wa viwanda ambavyo vitasukumwa na dawati hilo maalumu la viwanda, tutaweza kutimiza ndoto yetu ya Tanzania ya Viwanda” amesema Mhe. Nnauye

Akizungumza wakati wa mkutano huo Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi amesema kuwa ili vyombo vya habari viweze kutangaza habari vinahitaji kupata ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini kuonyesha mikakati na malengo ya serikali kuwezesha vyombo vya habari kujenga Tanzania ya viwanda na kuwapa fursa wananchi kupata taarifa sahihi za nchi. 

Naye Mtendaji kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Bibi. Mabe Masasi amesema kuwa Mapinduzi ya viwanda yanaweza kufanyika kama vyombo vya habari vitatoa taarifa sahihi za upatikanaji wa malighafi za uwekezaji kulingana na mahitaji yaliyopo katika maeneo husika na kuwekeza katika viwanda vidogovidogo vitakavyozalisha viwanda vikubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassani Abbas amesema kuwa atahakikisha maafisa habari wa serikali hususani maafisa wanaohusika na Sekta ya viwanda wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya habari ili kuweza kuelimisha umma namna Tanzania ya Viwanda inavyojengwa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiongea na wamiliki wa vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa  na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam. 
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari  nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas 
 Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa  na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.
 Mdau wa Habari Bw. Hamza Kasongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo 
Baadhi ya Wadau waliohudhuria mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA MICHUZI JR.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel
Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi
 Mwakilishi wa ITV/Radio One Steven Chua
 Mdau Mkubwa wa vyombo vya habari,Theophil Makunga

No comments: